• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI yatoa fidia ya bilioni 2.5 kupisha mradi wa umeme wa Grid Songea-Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: May 31st, 2025

Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeanza rasmi zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi waliopisha mradi mkubwa wa kusambaza umeme wa gridi ya taifa wenye nguvu ya kilovoti 220 kutoka Songea hadi Tunduru mkoani Ruvuma. Mradi huo wa kimkakati unaotarajiwa kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme vijijini na mijini, unatarajiwa kujengwa kwa urefu wa kilometa 264 ambapo takribani shilingi bilioni 2.5 zinatolewa kwa wakazi walioguswa.

Zoezi hilo limezinduliwa katika mtaa wa Mletele, Manispaa ya Songea ambapo zaidi ya wananchi 200 wameanza kulipwa fidia. Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa Tarafa wa Songea Mashariki, Dismas Komba amewataka wananchi waliopokea fidia kupisha mara moja maeneo yao ili serikali iendelee na ujenzi wa miundombinu ya umeme bila kuchelewa zaidi. “Ukishalipwa, toa mazao yako kama mahindi ambayo yameshaiva, usichukue muda mrefu. Tunaomba usaidie taifa kwa kuacha eneo bila usumbufu,” amesema Komba.

Afisa huyo pia aliwataka wananchi kutotumia fedha hizo vibaya kwa sababu ni sehemu ya mchango wao katika maendeleo ya nchi. “Msije mkazivunja ndoa zenu kwa sababu ya fidia, hizi fedha ni kwa ajili ya kupisha maendeleo. Nawaamini kuwa nyie ni watu wa kuelewa,” amesisitiza huku akipongeza ushirikiano kutoka kwa wananchi waliokwishalipwa.

Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa TANESCO mkoani Ruvuma, Aran Njilo, amewataka wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya mradi kushirikiana kikamilifu na mkandarasi pamoja na kuhakikisha miundombinu ya umeme inalindwa dhidi ya wizi na uharibifu. “Tunaomba wananchi mtambue huu ni mradi wa maendeleo. Mkandarasi ataendelea na kazi, hivyo ni muhimu tushirikiane na kulinda vifaa na miundombinu ili mradi huu uwe na tija inayotarajiwa,” amesema Njilo.

Mradi wa kusafirisha umeme wa Songea-Tunduru ni sehemu ya jitihada za serikali kupitia TANESCO kupanua mtandao wa umeme wa gridi ya taifa kuelekea Kusini mwa Tanzania. Kukamilika kwake kunatarajiwa kuondoa changamoto ya umeme  katika wilaya ya Tunduru na kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia sekta za viwanda, biashara na huduma.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.