Mafundi wameiomba kamati ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari kata ya Upolo Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kuwaongezea muda wa utekelezaji wa mradi huo kutokana na miundombinu mibovu ya barabara wakati wa kusomba vifaa vya ujenzi.
Akizungumza wakati akisoma taarifa mbele ya kamati ya siasa CCM Mkoa wa Ruvuma Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Khalid Kharif amesema mafundi wameomba kuongezewa muda kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza ikiwemo ya ukatikaji wa madaraja ya miti kwenye mito wakati wa kusomba vifaa vya ujenzi.
Amesema ujenzi huo unahusisha majengo ya vyumba vya madarasa nane, jengo la maabara, utawala, maktaba na Tehama, ambapo hadi mradi kukamilika utagharimu kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 560 iliyotoka Serikali kuu kupitia mradi wa SEQUIP.
Kharif amesema mradi ulianza kutekelezwa Agosti 14 2023 na ulitarajiwa kukamilishwa Septemba 2023 ambapo sasa mradi unatarajia kukamilika Oktoba 30 mwaka huu.
“Wananchi wameshiriki kufanya kazi za kukusanya mawe tripu 18 na kujaza kifusi ndani kwenye msingi tripu 64 kwa kazi hizo zinathamani ya kiasi cha fedha shilingi 3,880,000.00”, amesema Kharif.
Amezitaja changamoto wanazokumbana nazo kuwa ni Maji yaliyopo hayatoshelezi miundombinu mibovu ya madaraja ya mito ambayo yanatuunganisha na Wilaya ya Mbinga ambapo tunachukulia vifaa vya ujenzi na
Hata hivyo amesema kati ya fedha shilingi milioni 560 mpaka sasa zimetumika zaidi ya shilingi milioni 123 na wamebakiwa na kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 437.
Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Mohamed Ally imeridhishwa na utekelezaji wa mradi huo wa sekondari mpya ambapo wameagiza channgamoto zilizopo zipatiwe ufumbuzi wa haraka ili mradi uweze kukamilika.
Imeandikwa na Farida Baruti
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Oktoba 20,2023
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.