Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma İmeanza ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika Kata ya Namakambale. Mradi huu unatekelezwa na serikali kupitia Programu ya Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) na unatarajiwa kukamilika kwa gharama ya shilingi milioni 560.
Ujenzi huu ni ishara tosha ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu nchini.
Shule hii mpya itakuwa na miundombinu bora ikiwa ni pamoja na vyumba vya madarasa vya kutosha, maabara, maktaba, na vyoo vya kisasa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.