• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI yatoa milioni 893 kuboresha miundombinu shule za msingi Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: June 30th, 2023

SERIKALI imetoa shilingi milioni 893 kupitia mradi wa uboreshaji miundombinu ya shule za msingi (BOOST) katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt.Frederick Sagamiko wakati anatoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya BOOST kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas alipofanya ziara ya siku moja ya kukagua miradi hiyo.

Amesema fedha hizo zinatumika kutekeleza miradi ya BOOST katika shule saba za msingi ambazo amezitaja kuwa ni Kipera, Amani, Mbulani, Matogoro,Bombambili,Mkuzo na Ruhuwiko na kwamba utekelezaji wa mradi umeanza Mei 15,2023 na miradi yote imefikia hatua ya ukamilishaji.

Dkt.Sagamiko amesema kati ya fedha hizo,shilingi milioni 513 zinajenga shule mpya ya msingi Kipera katika Kata ya Ruvuma yenye  uwezo wa kuchukua wanafunzi 800 ambapo mradi unahusisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 16,matundu 18 ya vyoo na jengo la utawala.

“Shule ya msingi Amani imepokea shilingi milioni 66.3  kujenga madarasa mawili ya awali ya mfano,shule ya Mbulani milioni 77.1 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na shule ya Ruhuwiko milioni 77.1 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa,tunamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kutujengea miundombinu bora ya shule za msingi’’,alisema.

Shule nyingine zilizopokea fedha za BOOST amezitaja kuwa ni Matogoro,Bombambili na Mkuzo ambazo kila shule imepokea  milioni 53.1 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.

Akizungumza baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi Kipera na ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Ruhuwiko,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali  Laban Thomas ameupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa mradi huo.

“Marekebisho yale madogo madogo yaliyoonekana yarekebishwe,kwa ujumla miradi inakwenda vizuri hongereni sana,fundi aongeze kasi ili mradi ukamilike kwa wakati,hakikisheni shule hii mpya  ya msingi Kipera iwe ya mfano katika Mkoa wa Ruvuma’’,alisisitiza.

Ameagiza shule hiyo iwe na mazingira ya kuvutia yaliyopandwa maua,miti na bustani sanjari na kutengeneza njia za kupita wanafunzi hali ambayo itaweka mazingira rafiki ya kujifunza na kufundishia kwa walimu na wanafunzi.

Hata hivyo Kanali Thomas  ametoa rai kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Michael Mbano kuwaalika madiwani katika Halmashauri nyingine kufika katika Manispaa hiyo ili kujifunza  namna ya kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi.

Mwisho

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.