Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma imepokea kiasi cha shilingi milioni 995 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika shule za msingi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mheshimiwa Kelvin Mapunda amesema fedha hizo zimelekezwa kwenda kujenga Vyumba viwili vya madarasa na matundu matatu ya vyoo na kujenga shule mpya mbili za msingi katika kata za Matarawe na Mpepai.
“Kukamilika kwa ujenzi wa shule hizo kutapunguza msongamamo katika shule za maeneo hayo hivyo kuboresha elimu ya awali na msingi’’,alisisitiza Mapunda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Grace Quintine ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikiwepo Afya, Maji, Elimu na Miundombinu ya barabara katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.