• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI yatoa shilingi milioni 55 kujenga madarasa mawili ya awali Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: March 25th, 2023

,HALMASHAURI ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,imepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 55,824,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili ya Elimu ya Awali ya mfano katika shule ya msingi Ngahokora.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Neema Maghembe amesema fedha hizo zimetolewa na Ofisi ya Rais- TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwa ni fedha za utekelezaji wa mradi wa kuimarisha Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa Elimu ya Msingi kwa awamu ya pili (GPE-LANES II).

Amesema utekelezaji wa mradi huo utahusisha ujenzi wa madarasa mawili (02), ujenzi wa matundu manne (04) ya vyoo vya kawaida na matundu mawili (02) ya vyoo vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu, ununuzi au utengenezaji wa samani za ndani viti na meza, ununuzi wa matanki mawili (02), mikeka mitano (05), shubaka, bembea (michezo ya wanafunzi), maandalizi ya viwanja vya michezo, ununuzi wa kizima moto, kutengeneza mfereji wa maji pamoja na kigundua moto.

Ameongeza kuwa Mradi wa kuimarisha Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa Elimu ya Msingi Awamu ya Pili (GPE-LANES II) ni msaada, hivyo haupaswi kulipa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Vilevile Mkurugenzi Neema amebainisha kuwa kulingana na maelekezo ya Serikali, mradi huo utatekelezwa kwa kutumia Force Account na unatakiwa kukamilika kabla au ifikapo tarehe 15 Juni, 2023.  

Aidha, Uongozi wa Halmashauri unatoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kwa kuleta fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii hususani Elimu.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.