SERIKALI kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ikiwemo baiskeli na fimbo kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji kutimiza ndoto zao.
Wanafunzi hao ni Jackson Ndunguru darasa la saba kutoka shule ya msingi Lipaya, Ezekiel Mhagama darasa la tatu kutoka shule ya msingi Mbinga Mhalule na Boniface Ndomba darasa la awali kutoka shule ya Msingi Masangu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi hao wamemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kwa kuwasaidia vifaa hivyo ambavyo vitawarahisishia kufika shuleni kwa wakati na kuwahi masomo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.