SERIKALI imetoa Zaidi ya shilingi Bilioni 18 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, matundu ya vyoo, mabweni, maabara, pamoja na ukarabati wa shule kongwe.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge wakati akitaja mafanikio ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Songea.
Amesema Milioni 760,162,500 zimetumika katika ujenzi wa nyumba tano za wathibiti ubora wa elimu katika Halmashauri za Tunduru, Songea Manispaa, Songea DC, Nyasa pamoja na Mbinga.
‘’Ndugu wananchi wa Mkoa wa Ruvuma napenda kuwajulisha Mkoa umefanikiwa kujenga vyumba vya madarasa 500 ikiwa shule za sekondari 448 na shule shikizi 52, ujenzi wa mabweni matatu katika shule maalumu za Msingi zenye watoto wenye ulemavu kwa gharama ya Shilingi Bilioni 10.24 kupitia Mradi Na.5441 TCRP’’, amesema RC Ibuge.
Hata hivyo amesema kiasi cha fedha Bilioni 1.48 zimetumika katika ukarabati wa Chuo cha Ualimu Songea.
RC Ibuge amesema kiasi cha fedha Bilioni 1.26 zimetumika katika ukarabati wa Vyuo viwili vya Maendeleo ya Wananchi Nandembo FDC pamoja na Muhukulu FDC.
Ameongeza kuwa kiasi cha fedha Zaidi ya shilingi Bilioni 3 zimetumika katika ukarabati wa Shule kongwe za Sekondari Shule ya Wasichana Songea, Shule ya Wavulana Songea, Kigonsera pamoja na Tunduru.
Amesema kiasi cha fedha Zaidi ya shilingi Bilioni zimetumika katika ujenzi wa Vyuo vya VETA viwili vilivyopo katika Wilaya ya Nyasa na Namtumbo.
Tutaendelea kuwaletea mafanikio ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita katika Mkoa wa Ruvuma yaliyotajwa na Mkuu wa Mkoa katika habari zinazofuata kupitia tovuti yetu.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Aprili 01 2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.