MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Neema Maghembe amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni kumi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za Elimu Msingi,Elimu Sekondari,Kilimo,Afya na TASAF ambapo hadi kufikia Juni 2023 Halmashauri hiyo imepokea zaidi ya shilingi bilioni 9.4 sawa na asilimia 94.16.
Maghembe alikuwa anatoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ambaye alifanya ziara ya kikazi ya siku moja ya ukaguzi wa miradi sekta ya elimu katika sekondari ya Mpitimbi na Jenista Mhagama iliyojengwa kijiji cha Parangu ambapo serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioini mbili kujenga vyumba vya madarasa,mabweni na vyoo katika sekondari hizo
vyumba tisa vya madarasa katika sekondari ya Mpitimbi ambapo hadi sasa vyumba sita vimekamilika kwa asilimia 100 na vyumba vitatu vipo katika hatua ya kukamilisha ufungaji wa milango ili vianze kutumika
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.