Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Khalid Khalif ametembelea na kukagua eneo la ujenzi shule ya Sekondari ya Linga inayojengwa katika Kijiji cha Ngingama Wilayani Nyasa
Serikali imetoa shilingi milioni 560,552,827 Kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shule mpya ya kisasa Sekondari Linga, Kwa ajili ya kutatua changamoto ya wanafunzi waliokuwa wanasafiri umbali mrefu kwenda kusoma katika shule ya Sekondari Lituhi.
Wanafunzi wanatembea umbali wa kilometa 25 kufuata sekondari hiyo hivyo kuwa kero kwa wanafunzi .Akiwa katika eneo hilo amehakiki mipaka ya eneo hilo na kuzungumza na viongozi wa Kata na vijiji vya Lukali, Ngingama na Litumba kuhamba na kuwataka kushiriki kikamilifu zoezi la ujenzi wa Sekondari hiyo.
"Ninawahamasisha Wananchi kujitokeza Kwa wingi kushiriki kikamilifu Ujenzi huu wa Sekondari ya Linga Kwa kuwa Serikali imetatua changamoto iliyokuwa inatutesa Kwa muda mrefu.tunamshukuru mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kutuwezesha fedha za ujenzi wa shule hii’’,alisema.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.