Serikali imewaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya wananchi wa Kata ya Mpitimbi Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma baada ya kuboresha huduma za afya katika hospitali ya Halmashauri hiyo iliyojengwa Kijiji cha Mpitimbi.
Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Sera,Bunge na Uratibu Mheshimiwa Jenista Mhagama kwa niaba ya wananchi wa Mpitimbi amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huo.
“Nainua sauti ya moyo wa shukrani kwa Rais Samia kwa sababu kata ya Mpitimbi haikuwahi kuwa na ndoto ya kujengewa hospitali kubwa ya Wilaya’’,alisema.
Amesema wananchi wa Kata ya Mpitimbi na Tarafa ya Muhukuru matibabu yao ya kibingwa ilikuwa ni lazima wayapate kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Songea au Kwenda kwenye hospitali ya Rufaa ya Misheni ya Mtakatifu Joseph Peramiho.
Amesema Jimbo la Peramiho lina kata saba katika Tarafa ya Muhukuru ambazo sasa zitakuwa zinapata huduma za matibabu katika hospitali ya Mpitimbi na kwamba hospitali hiyo pia inatoa huduma kwa wananchi wa nchi Jirani ya Msumbiji ambao wanapakana na Jimbo la Peramiho katika Kijiji cha Mkenda kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Amesema serikali imeboresha majengo na kununua vifaa tiba vya kisasa ambavyo vinawezesha huduma za matibabu za kibingwa kutolewa katika hospitali hiyo.
Amesema madaktari bingwa wamefika katika hospitali hiyo kutoa huduma mbalimbali za kibingwa ambao wameanza kutoa huduma hizo kuanzia Mei 6 hadi 10 mwaka huu hivyo kutoa fursa kwa wananchi wa vijijini kupata huduma za matibabu za kibingwa.
Cathibet Mapunda Mkazi wa Kijiji cha Mpitimbi aliyekuwa na changamoto ya usikivu ameipongeza serikali kwa kuwapeleka madaktari bingwa katika hospitali hiyo ambapo ameweza kupata huduma za kibingwa na hivi sasa hali yake imerejea kama kawaida.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.