Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) Dkt.Sophia Kashenge akizungumza kwenye maadhimisho hayo amelitaja shamba la mbegu Namtumbo lenye ukubwa wa hekta 3,580.4 kuwa ni miongoni mwa mashamba 16 ya mbegu yenye jumla ya hekta 17,710.26.
Ameyataja mashamba hayo ya mbegu yanapatikana katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Ruvuma, Tanga, Pwani, Arusha, Tabora, Kigoma,Katavi na Geita na kwamba shamba la mbegu Namtumbo ni la pili kwa ukubwa hapa nchini likiwa na watumishi 15.
Amesema katika msimu wa mwaka 2023/2024,shamba la mbegu Namtumbo linatarajia kuzalisha mbegu Zaidi ya tani 1,275 za mazao mbalimbali yakiwemo mahindi na alizeti .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.