• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SHAMBA la miti TFS Mpepo Nyasa lapanda miti hekta 2,240

Imewekwa kuanzia tarehe: November 21st, 2022


SHAMBA la miti Mpepo linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wilayani Nyasa mkoani Ruvuma limefanikiwa kupanda miti hekta 2,240.

Akitoa taarifa ya shamba hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mhifadhi Mkuu wa Shamba hilo John Kimolo amesema kati ya hekta zilizopandwa,hekta 1440 zimepandwa  miti jamii ya misindano (pines) katika tarafa ya Mpepo wilayani Nyasa na Liwilikitesa wilayani Mbinga.

Kimolo amebainisha zaidi  kuwa  hekta 400 imepandwa miti jamii ya misaji (teak)  katika eneo la Liuli mwambao mwa ziwa Nyasa na kwamba miundombinu ya bustani tayari imesimikwa kwa ajili ya uzalishaji wa miche ya misaji katika maeneo ya Liuli na Ndongosi.

“Shamba lina bustani nne Mpepo,Ndongosi,Tunduru na Liuli yenye jumla ya miche ya miti1,130,000 ikijumuisha miche aina ya misindano na misaji’’,alisisitiza Kimolo.

Kulingana na Mhifadhi Mkuu huyo,shamba la miti Mpepo ni miongoni mwa mashamba 24 yanayosimamiwa na kuhudumiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania na kwamba shamba hilo lilianzishwa 2017/2018 likiwa na ukubwa wa hekta 2,017 ambapo hivi sasa shamba hilo lina ukubwa wa hekta 20,905.

Hata hivyo Kimolo amesema Shamba la miti Mpepo limefanikiwa kupata eneo lenye ukubwa wa hekta 50,000 wilayani Tunduru kwa ajili ya uanzishwaji wa shamba jipya la miti ambapo katika mwaka wa fedha 2022/2023 serikali imetenga bajeti ya kuanza upandaji miti hekta 100.

Amezitaja faida za shamba hilo kuwa ni chanzo cha mapato ya serikali kuu,kupatikana kwa ajira za muda 3000 kwa mwaka,Halmashauri kupata tozo mbalimbali na upatikanaji wa malighafi za viwandani.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya shamba hilo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewapongeza TFS kwa kufanya kazi kubwa ya kupanda miti ambayo amesema ni biashara kubwa kutokana na mahitaji makubwa ya mbao.

“Kilimo ambacho kinaondoa umasikini kwa haraka lakini kinahitaji Subira ni kilimo cha upandaji wa miti,ukiwa na hekari moja ya miti,baada ya miaka 15 utakapoanza kuvuna miti,ndipo utaona faida kubwa ya kilimo cha miti’’,alisisitiza RC Thomas.

Amesema maeneo mengi ambako wanapanda miti kibiashara wamepata maendeleo makubwa hivyo ametoa rai kwa wananchi mkoani Ruvuma kuwa sehemu ya wapandaji wa miti badala ya kuwaachia TFS pekee.

Hata hivyo katika kukabiliana na uchomaji moto hovyo,Mkuu wa Mkoa amewaasa wananchi kuacha tabia ya kuandaa mashamba yao kwa kutumia moto badala yake watumie njia nyingine ambazo hazina madhara kwenye misitu.

Imeandikwa na Albano Midelo

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Novemba 20,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.