SHIRIKA la all Mather Children kwa ufadhili wa mfuko wa Maendeleo ya Kanisa la Anglikana, Serikali ya Canada wametoa msaada wa vifaa vya kujikinga na UVIKO 19 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 35.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa na Katibu mtendaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Masasi Padri Phares Lihewe kwa Naibu Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii, jinsi, wazee na watoto Mwanaidi Ally Khamis ,wakati waziara yake ya siku nne katika Mkoa wa Ruvuma.
Lihewe amesema katika kipindi cha awamu ya pili mradi umechangia juhudi za Serikali katika kupambana na Janga la UVIKO 19 ,mradi umejikita katika kuboreshea watoa huduma mazingira rafiki ya kutoa huduma za afya,wanafunzi kuendelea kupata elimu kwa kuzingatia tahadhari ya Ugonjwa huo.
“Katika eneo hili jitihada kubwa za mradi zimeelekezwa katika usafi kwa kutoa matanki 28 ya lita 500 ,Sabuni za maji 1030 ,vitakasa mikono 210 , kwenye shule za Sekondari ikiwemo 13 za Wilaya ya Tunduru ikiwemo Frenk Weston”.
Hata hivyo amesema malengo makuu ya mradi huo ni kuchangia juhudi za serikali katika kujikinga na madhara yanayoweza kuletwa na mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO 19 kwa kuwawezesha watoa huduma za afya na wahudumu kuwa na uelewa,vifaa kinga na tiba katika tahadhali ya ugonjwa huo.
Kwa upande wake ,Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii,Jinsia wazee na watoto ameliopneza Shirika hilo kwa kutoa misaada kwa kuhudumia wanafunzi ili kujikinga na ugonjwa wa mlipuko wa UVIKO 19.
Naibu Waziri amesisitiza wananchi kuweka vifaa vya kunawia mikono kwa maji tililika,Vitakasa mikono katika makusanyiko na katika nyumba za kuishi na kuvaa barakoa na wazee wenye magonjwa kama kisukari,shinikizo la damu,kansa kuto jumuika katika misongamano isiyo ya lazima na kuendelea kufuata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa afya.
“Gonjwa hili la COVID 19 lipo na wananchi tunatakiwa tujikinge na kuondokana na tatizo hili,tuwasikilize wataalamu waafya, na wadau wa maendeleo waliopo nchini kuendelea kutoa misaada mbalimbali katika Nyanja mbalimbali na mashirika yasiyo ya kiserikali kutekeleza majukumu na huduma zao ili zinawafikia walengwa maana wengine katiba zao zinaonyesha kutoa misaada kwa wananchi lakini wakishafanikiwa hujinufaisha wenyewe”. Amesisitiza.
Imeandaliwa na Ofisi ya Afisa Habari
Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.