SHIRIKA la Compasion International lenye makao makuu yake jijini Arusha limetoa msaada wa vyandarua 250 vyenye thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Agustino Mji mwema Dayosisi ya Ruvuma.
Msaada huo umetolewa kwa watoto wanoaishi katika mazingira magumu ili kujikinga na ugonjwa wa Malaria.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Mjimwema Padre John Midelo amesema kati ya vyandarua hivyo,kituo cha Mjimwema kipata vyandarua 150 na kituo cha Lupapila kimepata vyandarua 100.
Mgeni rasmi katika hafla ya ugawaji wa vyandarua hivyo alikuwa ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Songea Afrosina Mwanja ambaye amewaasa wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mazuri kwa sababu watoto hao ni viongozi wa baada.
Mwanja pia amewataka wazazi na walezi kuhakikisha kuwa vyandarua vilivyotolewa vinatumika kwa watoto na siyo kwa wageni au watu wengine.
,,Akina mama na akina Baba tuwajali watoto tuondokane na mila kwamba tukiweka chakula mezani wale wakubwa mtoto atakula baadae, kunawa mkubwa mtoto anakuwa wa mwisho anakula uchafu hizo ni mila mbaya kwa watoto’’,alisisitiza.
Hata hivyo Mwanja ametoa rai kwa wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata haki zao zote msingi ili waweze kuwa na maisha bora na kujenga taifa lenye maadili .
Meneja wa CRDB B amechangia kituo hicho kiasi cha 200,000 kila mwezi kuanzia mwezi Juni hadi Desemba 2020 ambako ameagiza fedha hiyo itumike kwa watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho ili kutatua changamoto zao mbalimbali.
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB tawi la Songea ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kugawa vyandarua 100 katika kituo cha Lupapila amewaasa wazazi na walezi kuwajali na kuwasomesha watoto wao ili wapate elimu ambayo ndiyo urithi wa pekee katika maisha yao.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Padre John Midelo amelishukuru shirika la Compasion International linaloshirikiana na Makanisa ya kipentecoste na CCT kulea watoto katika Nyanja kuu nne Kiroho,Kimwili,Kiakili na kiuchumi.
Amesema watoto hao wanalelewa kuanzia umri wa miaka mitatu hadi sabaambao wanalelewa mpaka kufikia umri wa miaka 22 na kwamba mtoto atakayeendelea na masomo ya juu ataendelea kufadhiliwa mpaka chuo kikuu akiwa hajavuka miaka 22.
Padre Midelo amesema shirika hilo limeahidi kutoa bima ya afya watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu watapewa bima ya afya na mavazi,vifaa vya shule na chakula.
Hata hivyo amesema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya miundo mbinu ambapo hadi sasa watoto wanaosoma idadi yao ni 95 na kwamba wana upungufu wa madarasa na choo kimejengwa kwa gharama milioni saba lakini bado ujenzi wake haujakamilika.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi Noela chisokole amelipongeza shirika hilo pamoja na makanisa yanayoshirikiana kutoa masaada huo kwa watoto wao,ambapo amesema awali hali ilikuwa ngumu kwa upande wa mavazi,chakula vifaa vya shule na matibabu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Ruvuma songea
Julai 8,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.