Shule mpya ya Msingi Tinginya iliyopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ni moja ya mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Mpango wa Uboreshaji wa elimu ya awali na msingi kupitia prpgram ya BOOST unaofadhiliwa na Serikali.
Ujenzi wa shule hii umeleta matumaini makubwa kwa wakazi wa kijiji cha Tinginya na maeneo jirani, ambao kwa muda mrefu watoto wao walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata elimu katika shule za mbali. Shule hii ina vyumba vya madarasa vya kisasa, ofisi ya walimu, matundu ya vyoo, na samani za kisasa ambazo zimeimarisha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Kupitia mradi huu wa BOOST, Serikali imeonesha dhamira ya dhati ya kuboresha elimu ya msingi nchini kwa kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi ya kusoma katika mazingira rafiki na salama. .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.