MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge amechangisha harambee ya kiasi cha shilingi milioni 9 kwaajili ya ukarabati wa Miundombinu ya Shule ya Msingi Huduma.
Afisa Elimu Mkoa Juma Fulluge amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo katika harambee ya kuchangia shule hiyo iliyopo Kata ya Ruhuwiko Manispaa ya Songea inauhitaji wa shilingi Milioni 20 ili kukarabati majengo hayo.
Hata hivyo amesema harambee hiyo ni kwaajili ya ukarambati wa miundombinu iliyopo pamoja na ujenzi wa vyoo ili wanafunzi wapate mazingira rafiki ya kujisomea.
Mkoa wa Ruvuma umepata shilingi bilioni 4 kwaajili ya ujenzi shule ya Mkoa na kwa upande wa afya Serikali inahakikisha inajenga vituo vya Afya na Hospitali kwaajili ya Watanzania.
Fulluge amesema serikali ya awamu ya Sita inafanya kazi kubwa ya kuhakikisha ustawi wa wananchi wa Tanzania ikiwemo Mkoa wa Ruvuma fedha zilizoletwa katika ujenzi wa Madarasa ya Uviko 19 ni shilingi bilioni 10 na kujenga vyumba 500 za Sekondari.
Mkuu wa Shule ya Huduma Marcia Kapinga akisoma taarifa kwa mgeni rasmi amesema Shule ya Msingi Huduma ipo ndani ya eneo la Jeshi Kikosi 411KJ Ruhuwiko na ilijengwa kwaajili ya Wanajeshi kujiendeleza Kielimu mwaka 1978. Na kuzinduliwa na Hayati Mwalimu Nyerere..
Kapinga amesema kwasasa Shule ipo chini ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea na inahudumia wananchi wote wanaoishi katika eneo lililozungukwa na kambi ya Jeshi na inajumla ya Wanafunzi 1139.
Amesema shule inamafanikio ya ufaulu wa asilimia 99 kwa miaka mine mfulullizo na changamoto ikiwemo upungufu wa madarasa ,uhaba matundu 32 ya vyoo vya wanafunzi pamoja na uchakavu wa matundu 10,Upungufu wa madawati 138 yaliyopo ni machakavu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Februari 16,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.