• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SIMBA adimu Duniani aangamia Liparamba

Imewekwa kuanzia tarehe: April 16th, 2025

Katika kijiji kidogo cha  Mitomoni kata ya Mipotopoto, pembezoni mwa Pori la Akiba la Liparamba wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, simulizi ya nadra na ya kusikitisha imetokea simba mnweye rangi ya kahawia na nyeupe, kiumbe adimu anayepatikana katika maeneo machache sana duniani, ameuawa baada ya kuingia kwenye makazi ya watu na kusababisha taharuki kubwa.

Kwa muda mrefu, wakazi wa kijiji hicho wameishi kwa amani, wakifahamu kuwa hifadhi ya Liparamba ni jirani yao, lakini si hatari kwao. Lakini siku nne zilizopita, hali hiyo ilibadilika ghafla.

Diwani wa Kata ya Mipotopoto Mheshimiwa Said Mahamud, anasimulia tukio la mwananchi mmoja aliyenusurika kifo baada ya kukutana uso kwa uso na simba huyo porini.

 “Alikuwa njiani kutoka shambani, alipokutana na simba huyo. Aliweza kujiokoa kwa kupanda mti na kutumia matawi kujilinda, kabla ya simba huyo kuondoka,” anasema Mahamud.

Lakini kama tukio hilo halikutosha kuibua hofu, usiku wa kuamkia Aprili 15, simba huyo alifanya kile kinachoonekana kama shambulizi la kipekee, alipanda paa la nyumba, akashika mbwa, kubomoa dirisha, na hata kuchukua nguo kabla ya kutoweka gizani.

Kulingana na Diwani huyo Usiku uliofuata, simba huyo akaingia zizini na kuua kondoo watano na mbuzi mmoja wa mwananchi Said Njete.

Kilichofuata ni hatua ya haraka ya Serikali kupitia askari wa wanyamapori wa Pori la Akiba Liparamba waliowasili kutoka Mbinga.Baada ya ufuatiliaji, waliweza kumuua simba huyo na kuchukua ngozi yake.

Kwa mujibu wa diwani huyo, simba huyo alikuwa ni dume mwenye rangi  ya kahawia na nyeupe ,maelezo yanayowiana na tabia ya simba adimu duniani wanaopatikana tu katika Pori la Akiba la Liparamba.

 Inasemekana kuwa simba huyo alikuwa dhaifu na mwenye dalili za ugonjwa, jambo ambalo huenda lilimfanya kuvuka mipaka ya pori na kuingia kwenye makazi ya binadamu.

“Kwa miaka mingi hatujawahi kushuhudia simba wakiingia hadi nyumbani kwa watu. Hili ni tukio la kwanza la aina yake,” alisema Mheshimiwa Mahamud.

Wananchi wa Mipotopoto wameipongeza Serikali kwa hatua ya haraka iliyochukuliwa, wakisema kuwa simba huyo angeweza kuleta maafa makubwa iwapo asingedhibitiwa.

Askari wa wanyamapori wamewataka wananchi kutoa taarifa mapema kila wanapoona wanyama hatari ili kuzuia majanga makubwa.

Pori la Liparamba, ambalo linapakana na nchi ya Msumbiji, ni moja ya hazina za kipekee za taifa, likiwa na mandhari ya kuvutia na wanyama adimu kama tembo na simba weupe wa ajabu, pori hili linatajwa kuwa na uwezo wa kugeuka kuwa moja ya vivutio vikuu vya utalii wa kipekee barani Afrika.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.