“Sitaandika barua ya kuomba chakula kwamba tuna njaa wakati juzi nimetoka kupokea Tuzo kwa Mheshimiwa Rais ya Mkoa wa Ruvuma kushika nafasi ya kwanza kwa uzalishaji wa mazao ya nafaka nchini”,alisema Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas wakati anazungumza na wananchi wa Kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea.
Amesema takwimu zinaonesha kuwa kwa miaka 13 mfululizo Mkoa wa Ruvuma unaongoza kwa uzalishaji wa chakula nchini ambapo amewataka wananchi kutouza chakula chote kwa tamaa ya fedha.
Mkuu wa Mkoa pia amewaagiza viongozi na wananchi wa mji wa Songea kuimarisha usafi wa mazingira kwenye mitaa yote ili manispaa ya Songea iwe na mandhari za kuvutia.
Kanali Thomas pia ametoa rai kwa wananchi mkoani Ruvuma kujiunga na Bima ya afya iliyoboreshwa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.