Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanakamilisha ujenzi wa soko jipya la kimataifa la madini ya vito .
Murungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Chiza Marando amelitaja soko hilo kuwa litakuwa soko kubwa zaidi Afrika Mashariki katika madini ya vito.
“ujenzi wa soko hili ulioanza Desemba 2023 unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Aprili 2024, mradi unagharimu zaidi ya shilingi bilioni moja “,alisema
Amebainisha zaidi kuwa soko hilo litakuwa na uwezo wa kutumiwa na Kampuni 155 za madini ya vito kwa wakati mmoja.
Hata hivyo amesema hadi sasa kampuni 130 zimeshaomba nafasi ya kufanya biashara kwenye soko hilo na kwamba eneo la soko lina uwezo wa kubeba kampuni zaidi ya 500.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Wakili Julius Mtatiro ameupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa maamuzi ya kujenga soko la madini lenye hadhi ya kimataifa.
Amesisitiza kuwa soko hilo litakuwa na tija katika rasilimali za madini ya vito zilizopo hapa nchini .
DC Mtatiro ameiagiza Halmashauri ya Tunduru kukamilisha haraka ujenzi huo na kuhakikisha soko linaanza kufanya kazi kwa wakati.
Amesema soko hili la pamoja likianza litapunguza vitendo vya utoroshaji wa madini ya vito wilayani humo, ambavyo vinafanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.
Hata hivyo ametahadharisha kuwa soko hili likianza serikali haitaruhusu tena masoko madogo madogo kama TUDECO na GENERATİON kuendelea na kazi kwani utitiri wa masoko hayo umekuwa chanzo cha utoroshaji wa madini ya vito.
Afisa Migodi wa Wilaya ya Tunduru Emmanuel Bushi amelitaja Soko Jipya la Pamoja la Kimataifa la Madini ya Vito litakuwa mkombozi wa wachimbaji wadogo kwa kuwa watapata ushindani na bei zenye tija,
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.