TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilayani Nyasa imewataka viongozi wa Halmashauri pamoja na madiwani kuongeza juhudi katika usimamizi wa ujenzi wa miradi ya maendeleo
Maagizo hayo yametolewa na Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Nyasa Dinioz Sylvanus katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo wakati wa kujadili taarifa ya robo nne ya (April-June 2023) kilichofanyika ukumbi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri.
Amesema viongozi wanawajibu mkubwa wa kusimamia fedha za wananchi zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi, hivyo ni wajibu wa viongozi wa miradi pamoja na wataalamu kusimamia na kufuatilia kwa karibu ujenzi wa miradi hiyo
“Usimamizi wa miradi ni kazi ya viongozi pamoja na wataalamu haipendezi kuona kiongozi mkubwa anakuja na kukuta dosari ambayo sisi ndio tupo karibu na miradi hiyo tushirikiane katika swala utendaji kazi ili kuepusha kufuatana kwa kuchunguzana pale dosari zinapojitokeza niwaombe tuweke uzalendo mbele”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.