• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TAKUKURU RUVUMA yabaini mapungufu miradi mitano ya maendeleo

Imewekwa kuanzia tarehe: May 18th, 2023

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imebaini mapungufu katika utekelezaji wa miradi mitano ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5.5.

Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi 2023 kwa wanahabari,Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Janeth Haule,amesema hatua mbalimbali zilichukuliwa ili kuondoa mapungufu hayo kwenye miradi hiyo.

Hata hivyo amesema katika kipindi hicho TAKUKURU ilifuatilia utekelezaji wa miradi 15 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6.5.

Ameitaja miradi iliyobainika kuwa na mapungufu kuwa ni mradi wa ujenzi wa madarasa tisa katika shule ya sekondari Sasawala wilayani Namtumbo wenye thamani ya shilingi milioni 180,ambapo TAKUKURU ilibaini mradi kuchelewa kukamilika kutokana na ucheleweshaji wa ununuzi wa vifaa na mafundi.

“TAKUKURU tulitoa ushauri kwa Halmashauri kutoa ukomo wa bei kwa wazabuni na kufanya malipo kwa wakati baada ya kujiridhisha na uchunguzi’’,alisisitiza Haule.

Kulingana na Naibu Mkuu wa TAKUKURU,ameutaja mradi mwingine waliobaini mapungufu kuwa ni ujenzi wa majengo matatu katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo unaogharimu shilingi milioni 800,ambapo walibaini mradi kuchelewa kukamilika ambapo TAKUKURU ilishauri kufanya tathimini sahihi ya vifaa na kufanya manunuzi ya jumla.

Haule ameutaja mradi mwingine waliobaini mapungufu ni ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD)  katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea unaogharimu shilingi bilioni 3.87 ambapo TAKUKURU ilibaini kuchelewa kukamilika kwa mradi, ucheleweshaji wa makabidhiano na mradi kufanyika kwa awamu mbili.

Amesema TAKUKURU ilishauri kukamilishwa haraka kwa mradi huo katika awamu ya pili ili kuepuka upotevu wa vifaa vya ujenzi kutokana na kurudia kazi moja mara mbili.

Miradi mingine iliyogundulika kuwa na mapungufu ni ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Mbinga unaogharimu shilingi milioni 500 na ujenzi wa kituo cha afya Kata ya  Mbangamao Mbinga unaogharimu shilingi milioni 250.

Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma amesema katika kipindi hicho  TAKUKURU ilipokea malalamiko 20 kati ya hayo malalamiko tisa ni ya rushwa na kwamba  TAKUKURU iliweza kutoa elimu kupitia semina 26,klabu za wapinga rushwa 70 za shule za msingi na sekondari,mikutano ya hadhara 11,vipindi vya redio vinne,Makala saba na maonesho saba.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Mei 18,2023 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.