Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Ruvuma imefanikiwa kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo 46 yenye thamani ya jumla ya sh. Bilioni 11.025, ambapo miradi 17 yenye thamani ya sh. Bilioni 5.9 ilikutwa na mapungufu.
Changamoto zilizobainika ni pamoja na uandishi mbovu wa nyaraka (store ledger) unaosababisha upotevu wa vifaa vya ujenzi, miradi kuchelewa kuanza kutokana na mafundi wengi kutofahamu kutumia mfumo mpya wa NEST.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma, Hamza Mwenda, alizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mahenge mjini Songea,amesema changamoto hizo ziliwasilishwa kwenye halmashauri husika ili kutafutiwa ufumbuzi, baadhi zikiratibiwa na zingine zikiendelea kufanyiwa kazi.
Ameitaja miradi yenye mapungufu ni pamoja na Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu 6 ya vyoo shule ya msingi Magingo, Ujenzi wa madarasa 6 na mabweni 2, sekondari ya Madaba, pamoja na miradi mingine ya ujenzi wa shule mpya za sekondari na mahakama ya Wilaya ya Tunduru.
Amesema TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imepokea jumla ya malalamiko 76 kutoka kwa wananchi kuanzia Oktoba hadi Disemba 2024, ambapo malalamiko 53 yaliyohusu rushwa yameshughulikiwa na uchunguzi ukiendelea. Katika kipindi hicho, TAKUKURU imefungua kesi mpya 15, na kesi 10 zimetolewa maamuzi ambapo upande wa Jamuhuri umeshinda.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.