Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Ruvuma Imeokoa mifuko 100 ya saruji katika mradi wa ujenzi wa zahanati ya Masimeli katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga.
Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa TAKUKURU katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi 2020,Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma, Yustina Chagaka amesema Mifuko hiyo ilikuwa mbioni kuibiwa na baadhi ya viongozi wa kata ya kitanda katika Halmashauri hiyo.
Amesema baada ya TAKUKURU kubaini njama hizo iliamua mifuko hiyo ya saruji irejeshwe katika Halmashauri ya mji wa Mbinga.
Chagaka amesema Halmashauri ya mji wa Mbinga ilipeleka saruji mifuko 120 kaitka mradi huo ambapo mahitaji ni mifuko 240 lakini kuna fedha ambayo ilitolewa na Mhisani kutoka Ujerumani kiasi cha Euro 10,000 sawa milioni 24 kwa kata ya Kitanda.
“Tumejipanga kuendelea kuelimisha wananchi kupiga vita rushwa katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwisho mwa mwaka 2020 ili wananchi wafahamu thamani ya kura zao na umuhimu wa kuchaguwa viongozi bora.” Amesema Chagaka.
Katika hatua nyingine, TAKUKURU wameokoa jumla ya fedha zaidi ya milioni 554,ambazo zimetokana na uchunguzi mbalimbali ambao unaendelea kufanywa na TAKUKURU.
Amesema kati ya fedha hizo zaidi ya milioni 498, zimeokolewa kutokana na uchunguzi wa vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS)Wilaya ya Songea.
Hata hivyo kiasi cha fedha zaidi ya milioni 10,zimeokolewa kutokana na uchunguzi uliofanyika katika vyama vya ushirika (AMCOS) Wilayani Namtumbo ambapo fedha hizo zimekabidhiwa kwa wakulima waliokuwa wamedhulumiwa mazao yao.
Chakaga amesema zaidi ya milioni 1.6 ,ni fedha ambazo zimerejeshwa baada ya uchunguzi katika mfuko wa TASAF Wilayani Tunduru baaada ya kubaini kwamba baadhi ya watumishi walikuwa wakijilipa posho isivyohalali.
Imeandikwa na Farida Mussa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.