TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imetoa mafunzo ya namna ya kuripoti habari za uchaguzi Mkuu unaoatarajia kufanyika Jumatano Oktoba 28 mwaka huu.
Mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, yametolewa na Mwanasheria wa TAKUKURU Herman Malima.
Malima amesema waandishi wa habari wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi madhara ya kupata viongozi kwa njia ya rushwa na kuwa mfano wa kuigwa katika mapambano dhidi ya rushwa kwasababu wao ni kioo cha jamii.
Amesisitiza kwa waandishi wa habari wasiandike taarifa ambazo zinaleta uchochezi kwa wanasiasa na jamii kwa sababu kwa kufanya hivyo wanaweza kuleta machafuko na ukosefu wa amani katika Taifa letu la Tanzania.
“Sheria ya uchaguzi namba moja ya mwaka 1985 inahusika na kuongoza chaguzi za Rais,Wabunge na Madiwani,Sheria inatoa taratibu za uchaguzi na mamlaka mbalimbali ikiwemo kuanzishwa kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC),Sheria hii inakemea vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi na inaelekeza adhabu”.amesema Malima
Mwanasheria huyo ameonya viongozi wanaopitishwa kwa njia ya Rushwa hawafai kwa sababu wanaweza kusababisha kudumaza uchumi wa Taifa kutokana kuwa na watakuwa viongozi wasiopambana na rushwa kwa ukamilifu.
Akizungumza wakati anafungua mafunzo hayo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda ametoa rai kwa wanahabari kuhakikisha kuwa wanaripoti habari za uchaguzi kwa weledi na maadili ili kutosababisha machafuko katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Amesema mafunzo hayo yataongeza umakini na uangalifu katika kutafuta,kuchuja na kusambaza habari mbalimbali zitakazokuwa zinaandikwa katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Imeandaliwa na Farida Baruti na Aneth ndonde
Kutoka ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Oktoba 22,2020.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.