• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TAKUKURU Ruvuma yawafunda wanahabari madhara ya rushwa kwenye uchaguzi

Imewekwa kuanzia tarehe: August 23rd, 2024

Na Albano Midelo

MIONGONI mwa madhara makubwa ya rushwa kwenye uchaguzi yametajwa kuwa ni kunyima haki ya kuchagua kiongozi bora na anayehitajika  hivyo kukwamisha maendeleo kutokana na viongozi waliopatikana kwa njia ya rushwa.

Hayo yamesemwa na Afisa wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yahaya Mwinyi  wakati anatoa mada ya nafasi ya wanahabari katika mapambano ya rushwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 2024 na uchaguzi Mkuu 2025.

TAKUKURU wameandaa mafunzo hayo kwa wanahabari 21 kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wilayani Songea  ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa TAKUKURU Mahenge Manispaa ya Songea.

Mwinyi ameyataja madhara mengine ya rushwa kwenye uchaguzi kuwa ni  wananchi wanadharirika kwa kuthaminishwa na vitu vidogo kama pombe na zawadi ili kuwachagua viongozi wasiokuwa na sifa hivyo jamii kukosa huduma muhimu kama zahanati,umeme na maji.

“Madhara ya rushwa kwenye uchaguzi,wananchi kupata viongozi wasiokuwa waadilifu na kuongezeka kwa umasikini kwa sababu viongozi waliochaguliwa wanakosa sifa za kuwaletea maendeleo wananchi’’.alisisitiza Mwinyi.

Awali akizungumza kwenye ufunguzi na ufungaji wa mafunzo hayo Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Janeth Haule amesema TAKUKURU imeamua kufanya  mafunzo hayo kwa wanahabari kwa kutambua  Taifa linaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Amesema wanahabari wana mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya rushwa kwa sababu  wanahabari ni kioo cha jamii na wana uwezo mkubwa wa kuwafikia wananchi wengi kwa haraka.

“Vyombo vya Habari vinaaminika sana kwa wananchi kwa hiyo tumeona tuanze kutoa mafunzo haya kwanza kwa wanahabari na baadaye tutaingia katika makundi mengine’’,alisema Haule.

Amesisitiza kuwa vyombo vya Habari vina nafasi kubwa ya kuzuia rushwa kwenye uchaguzi  hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ameutaja wajibu wa vyombo vya Habari hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ni kubadili fikra za wananchi kulingana na misingi ya maadili,uadilifu,utawala bora,haki za binadamu,uzalendo na upendo.

Amesema rushwa inakatazwa kila mahali ambapo kisheria rushwa ni kosa la jinai,rushwa pia ni utovu wa maadili kwa jamii na  dini zote zimetamka wazi kuwa rushwa ni dhambi.

TAKUKURU Ruvuma itaendelea na uelimishaji wa madhara ya rushwa kwenye uchaguzi kwa kutoa elimu katika makundi mbalimbali yakiwemo wanahabari,viongozi wa dini,viongozi wa vyama vya siasa na kuendelea kuwaelimisha wananchi kwa ujumla kuhusu mapambano dhidi ya rushwa kuelekea kwenye uchaguzi  

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.