• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TAKUKURU yasaidia kupatikana kwa mapato Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: May 30th, 2025

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Ruvuma imefanikiwa kuwezesha upatikanaji wa fedha za makusanyo ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma,  Janeth F. Haule, mafanikio hayo yamepatikana kupitia utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2025.

Imeelezwa kuwa jumla ya Shilingi 9,205,158.44 zilizotokana na makusanyo ya mapato kutoka vyanzo mbalimbali vilivyokusanywa na mawakala kwa njia ya mifumo ya kielektroniki, hazikuwasilishwa benki kama taratibu zinavyotaka. Hata hivyo, baada ya TAKUKURU kufanya ufuatiliaji wa karibu, fedha hizo hatimaye ziliwasilishwa benki.

Aidha, ufuatiliaji huo umechochea ongezeko la makusanyo ya mapato katika Halmashauri hiyo, hususan kwenye Divisheni za Kilimo, Mifugo na Uvuvi; Biashara; Ardhi na Maliasili, ambapo kiwango cha makusanyo kimepanda kutoka asilimia 50 hadi kufikia asilimia 102 kupitia mifumo ya kielektroniki.

TAKUKURU imetoa ushauri wa marekebisho kwenye miradi mitatu (3) ya sekta za Miundombinu, Kilimo na Fedha, yenye jumla ya thamani ya Shilingi 29,917,135,361.43, baada ya kubaini mapungufu katika utekelezaji wake.

Katika kipindi hicho cha Januari – Machi 2025, TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imefanya chambuzi tatu (3) na kuendesha warsha tatu (3) na wadau mbalimbali, ambazo zimesababisha kufikiwa kwa maazimio 16 ya kuziba mianya ya rushwa. Programu hizi zinatekelezwa katika kata 12, ambapo jumla ya kero 118 zilibainika, kati ya hizo kero 89 zimetatuliwa na kero 29 zinaendelea kushughulikiwa.

Aidha TAKUKURU imefanya Semina 24, Uimarishaji wa klabu za wapinga rushwa 53, Mikutano ya hadhara 26, Maonesho 06, Makala 02 na Vipindi vya Redio 03 ikiwa pamoja na Malalamiko 100 yalipokelewa, Kati ya hayo, 80 yalihusu rushwa na 20 hayakuhusu rushwa huku Kesi 04 zilifunguliwa Mahakamani ambapo kesi 03 zimetolewa Hukumu na Jamhuri imeshinda kesi zote 03 na hakuna kesi iliyoshindwa.

Akihitimisha taarifa yake, Janeth Haule ametoa wito kwa wananchi kujitayarisha na kushiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa kuepuka vitendo vya rushwa ili kuhakikisha taifa linapata viongozi waadilifu, watakaowezesha maendeleo na kudumisha amani nchini

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.