Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Ruvuma imetoa taarifa kuhusu utendaji kazi wake wa mienzi mitatu kuanzia Julai hadi Septemba
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo Novemba 29, 2022 Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Bi Janeth Haule katika ofisi yao iliyopo mtaa wa mahenge Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma
Amesema TAKUKURU katika kipindi cha mienzi mitatu iliendelea kutekeleza majukumu yake kufanya uchunguzi wa makosa ya rushwa na kuwafikisha mahakamani wale waliobainika na kujihusisha na vitendo vya rushwa katika mifumo ya taasisi za umma na sekta binafsi
Amesema kwa kipindi cha mienzi mitatu taasisi hiyo imefuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye thamani ya Zaidi ya shilingi bilioni 6.3 na ufuatiliaji huo imefanyika katika Wilaya ya Songea, Mbinga na Tunduru
Pia ameeleza kuwa TAKUKURU katika ufuataliaji imebaini ujenzi wa maradi wa Barabara Manispaa ya Songea pamoja na Halmshauri ya Wilaya ya Mbinga wenye thamani ya shilingi bilioni 5.7 kukusekana kwa vivuko vya watumiaji barabara katika maeneo ya wazi
Amesema ujenzi wa nyumba za watumishi Wilaya ya Nyasa zenye thamani ya shilingi milioni 90 wamebaini kuwepo na kasi ndogo ya kuleta matofali kutoka kwa mtu aliyepewa wa Nyasa pamoja na Wilaya ya Tunduru kwenye mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Wilaya wenye thamani ya shilingi milioni 470 wamebaini mafundi walikuwa wameanza kufanya kazi bila kusaini mikataba yao ya kazi
Hata hivyo TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma amefanikiwa kufanya kazi mbili za uchambuzi za usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika idara ya elimu misingi wa sekondari katika manispaa ya Songea
Amesema wajumbe wakamati za ujenzi , manunuzi na mapokezi kupangwa katika kamati Zaidi ya moja pia upandishaji wa bei ya vifaa vya ujenzi unaofanywa na wajumbe wa kamati na baadhi wa wazabuni wasio kuwa waadilifu pia vifaa vya ujenzi kupokelewa bila kukaguliwa na Mhandisi
Pia uchambuzi wa mfumo wa ukusanyaji yatokanayo na ushuru wa makaa ya mawe katika Wilaya ya Mbinga wamebaini yapo magari ambayo yamewai kupita bila kulipa ushuru yakafukuziwa yakalipa ushuru pasipo kutozwa kodi
Amesema TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha mienzi mitatu ijayo kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba wamejipanga kuelimisha wananchi juu ya rushwa na madhara yake katika usimamizi wa miradi ya maendeleo lengo kuwawezesha kupata uelewa na kuweza kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa karibu na weledi wa hali ya juu
Amewasisitiza wananchi waendelee kushirikiana na TAKUKURU kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa pia nao kama TAKUKURU wataendelea na zoezi la kutembelea wananchi katika maeneo yao kwa lengo la kusikiliza kero za rushwa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.