Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Peres Magiri amezindua Tamasha kubwa la Toyota Festival ambalo limelenga juhudi za kuimarisha utalii, kukuza uchumi wa Mkoa huo na kuhamasisha ushirikiano wa kijamii kupitia shughuli mbalimbali za kibiashara na kijamii.
Mkuu wa Wilaya huyo ambaye amemwakilisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed alisema hayo wakati wa uzinduzi wa Toyota Networking cocktail iliyofanyika Disemba 7mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano Anglikana manispaa ya Songea.
Alisema kuwa Tamasha hilo ambalo linatarajia kuwa na maandamano ya magari aina ya Toyota zaidi ya 5000 kutoka Songea hadi Mbambabay wilayani Nyasa inatarajiwa kufanyika Juni 2025.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Peres Magiri akizindua Tamasha la Toyota festival mkoani Ruvuma.
“Tamasha hilo litajumuisha maonesho ya magari ya Toyota ,shughuli za Burudani,maonesho ya bidhaa mbalimbali pamoja na fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Mkoa wetu wa Ruvuma”alisema mkuu huyo wa Wilaya Magiri.
Alisema lengo la tamasha hilo ni kuhakikisha tamasha linakuwa na fursa nzuri ya kuonesha rasilimali za kiutalii na kiuchumi zinazo patikana katika Mkoa huo.
Hata hivyo amewakaribisha wawekezaji, Taasisi mbalimbali na wananchi kushiriki kwenye tamasha hilo ili kuongeza nafasi za ajira na kukuza maendeleo ya kiuchumi.
Kwa upande wake KatibuTawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo amesema kuwa Tamasha la Toyota festival litasaidia kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya Mkoa huo na kwamba litakusanya watu kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania
. Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo akizungumza kwenye uzinduzi wa Tamasha la Toyota festival lililofanyika katika ukumbi wa mikutano Anglikana Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Alisema kuwa serikali inatumia magari aina ya Toyota hivyo wanawaharika watu mbalimbali toka ndani na nje ya nchi kushiriki na kufadhili Tamasha hilo hivyo wawe mstari wa mbele kuhakikisha wanafanikisha.
“Ni imani yangu kuwa tutaendelea kushirikiana katika maandalizi ya Tamasha hili ili kutangaza utalii wa Mkoa wa Ruvuma ambalo linatarajiwa Kufanyika mwezi juni mwakani ambapo wadau mbalimbali wa utalii toka ndani na nje ya Mkoa wa Ruvuma wanakaribishwa kufadhili ,”Alisema Makondo.
Mwakilishi wa kampuni ya Toyata Mkoa wa Ruvuma,Wakili John Njau alisema kuwa Toyota wameweza kuuza Magari na vipuri mbalimbali ambapo Tamasha hilo la Toyota festival ni Tamasha ambalo linawaweka wananchi pamoja na si vinginevyo.
Naye Kamanda wa wakala wa misitu (TFS )Kanda ya kusini Manisie Mpokigwa,amesema kuwa Taasisi yake inafanya kazi ya kutangaza utalii wa vivutio mbalimbali hivyo Tamasha hilo litasaidia kutangaza utalii wa Mkoa wa Ruvuma ikiwemo Misitu ya hifadhi ya chanzo cha mto Ruvuma kilichop Milima ya Matogoro lakini pia wanautajiri wa hali ya juu katika mapori ya TANAPA na TAWA hivyo watalii wengi wameongezeka
Maajabu Mbogo muhifadhi toka TAWA, Mkoa wa Ruvuma amesema kuwa Mkoa wa Ruvuma umejaliwa vivutio vingi vya utalii ikiwemo hifadhii ya Nyerere,kisiwa Cha Lundo ambapo Kuna samaki wa urembo zaidi ya 400, makumbusho ya maji maji ,fukwe za ziwa Nyasa,milima Matogoro,na vivutio vingine vingi.
Titos Kajungu ofisa Masoko toka kampuni ya Wategi wamekuja na wazo la kutangaza vivutio vya utalii vya Mkoa wa Ruvuma ambavyo ni vya kipekee na wameamua kuwa na mkakati mzuri wa kushirikiana na Serikali kuendelea kuhamasisha utalii na wataendelea kuvitangaza vivutio vilivyopo Mkoa wa Ruvuma ili wajue uzuri wa Mkoa na Nchi kwa ujumla.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.