TAMASHA la Utamaduni la Kitaifa la tatu linatarajia kufanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma kuanzia Julai 20 hadi 27 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo Joel Mbewa amesema tamasha la kwanza la kitaifa la utamaduni lilifanyika mkoani Dar es salaam mwaka 2022 na tamasha la pili lilifanyika mkoani Njombe mwaka 2023.
Amesema katika matamasha hayo mawili ya kitaifa Mkoa wa Ruvuma ulifanikiwa kushika nafasi ya sita kitaifa kati ya mikoa 31 ya Tanzania Bara na visiwani.
“Kwa kuwa tamasha hili mwaka huu kitaifa linafanyika mkoani Ruvuma,tumedhamiria kufanya vizuri Zaidi ikiwezekana kushika nafasi ya kwanza kitaifa kati ya mikoa 31 inayoshiriki kwenye tamasha hilo’’,alisisitiza.
Tamasha la kitaifa la utamaduni lilianzishwa mwaka 2022 ikiwa ni kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa alipokuwa mgeni rasmi mkoani Mwanza Septemba 8,2021 katika Tamasha la utamaduni la Bulabo.
Rais Samia aliagiza matamasha ya utamaduni kufanyika kwa mzunguko kila Mkoa ili watanzania wajue mila na desturi za kila Mkoa ambapo aliagiza kuwe na mashindano ya ngoma za asili na washindi wapewe Tuzo.
Malengo makuu ya tamasha la kitaifa la utamaduni ni kurithisha amali za utamaduni kwa vitendo, kuchochea maendeleo ya utalii wa kiutamaduni, Sanaa za asili,sekta za ubunifu wa asili, kuhamasisha utaifa,uzalendo na urithishaji wa maadili kwa mtanzania
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.