Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imekabidhi pikipiki kwa watendaji wa Kata tatu za Mpepo,Mbambabay na Liwundi ili kuongeza uwajibikaji kwa wananchi.
Pikipiki hizo zimekabidhiwa kwa watendaji hao na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa Khalid Khalif amewataka watendaji hao wafanye kazi kwa juhudi na kuongeza uwajibikaji kwa wananchi,ikiwa ni Pamoja na kutatua kero za wananchi.
Pikipiki hizo zimetoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI na zimeletwa kwa ajili ya watendaji hao ili waweze kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi.
Amemshukuru Mhe. Dkt Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa usafiri wa Pikipiki hizo.
Wakizungumza baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo,Hiram Malugu ni Mtendaji Kata ya Mbamba bay ambaye amesema alikuwa anatumia pesa ya mfukoni kwa ajili ya kwenda kutatua changamoto za wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.