• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TAMKO la Kamati ya Mahusiano ya Dini Mkoa wa Ruvuma,kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28

Imewekwa kuanzia tarehe: October 21st, 2020

WATANZANIA wametakiwa kutambua umuhimu wa  kujitokeza kuchagua viongozi ngazi mbalimbali kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Rai hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Dini mkoani Ruvuma Shekh Ally Hassan Mahaba,wakati Kamati hiyo inatoa tamko  kuelekea Uchaguzi Mkuu kwa wanahabari   kwenye ukumbi wa Ruhuwiko Hunt Club  mjini Songea.

Shekh Mahaba  ameyataja matamko ya  Kamati ya Dini Mkoa wa Ruvuma kuwa ni kuombea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu na kusimamia amani na upendo wa nchi.

Amesema katika kuhakikisha zoezi la uchaguzi Mkuu linafanyika kwa amani,Kamati ya Mahusiano ya Dini mkoani Ruvuma imeweka utaratibu wa kuombea uchaguzi kwenye misikiti na makanisa siku mbili ambazo ni Oktoba 23 na Oktoba 25 mwaka huu.

“Tumeendelea kusisitiza kwamba,waumini wetu na wasiokuwa waumini   Oktoba 28 mwaka huu,wakishapiga kura warudi nyumbani  kupumzika ,wakisubiri matokeo ’’,alisisitiza Shekh Mahaba.

Makamu Mwenyekiti huyo amesisitiza  kuwa isitokee vurugu baada ya wananchi kupiga kura na kwamba kupiga kura ni suala la siri ambapo ameitaja kazi kubwa ya viongozi wa dini ni kuhubiri upendo,mshikamano,amani,na ushirikiano.

Ametoa rai kwa wasimamizi wa uchaguzi kufanyakazi kwa weledi na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum kama wenye ulemavu ili waweze kujaza fomu zao vizuri kwenye vituo vya kupigia kura.

Amewaasa viongozi wa dini wasijihusishe na kuelekeza waumini kwamba apigiwe kura mgombea Fulani katika kipindi hiki.

Kwa upande wake Katibu wa Kamati ya Mahusiano ya Dini Mkoa wa Ruvuma Alhaj Abdalah Mohamed Ndesai  amesema Kamati  imedhamiria kuhubiri amani na utulivu kila wakati ili Tanzania iendelee kuwa kisiwa na amani.

Amesema nchi inapoingia kwenye uchaguzi Mkuu,viongozi wote wa dini wanapaswa kuwaeleza waumini umuhimu wa kwenda kupiga kura kwa sababu ni haki na Katibu ya nchi inaruhusu kila baada ya miaka mitano kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu.

Mackei Mguhi ni Mjumbe wa Kamati ya Mahusiano  ya Dini toka Kanisa la Anglikana,amesema Tanzania imekuwa na amani  kwa miaka yote, hivyo hatutegemei katika uchaguzi wa safari hii mambo kuwa tofauti ambapo amesisitiza viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani na upendo kabla na baada ya uchaguzi.

 Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Ruvuma  Fatuma Misango  ameunga mkono tamko la viongozi wa dini akisisitiza kuwa kila mpigakura anatakiwa kujua wajibu wake wa kwenda kupiga kura na kurudi nyumbani lengo likiwa ni kudumisha amani ya nchi iliyopo.

Amesema hakuna dini yeyote ambayo inahamasisha upotevu wa amani na kwamba amani ikitoweka ni vigumu kuirudisha hivyo ameshauri kufuata sheria za uchaguzi ili kulinda amani na utulivu wa nchi.

Mbwana Said Mjumbe ni Mjumbe toka Baraza la BAKWATA Mkoa wa Ruvuma amewahimiza watanzania kujitokeza kuwachagua madiwani,wabunge na Rais Oktoba 28 mwaka huu na kuendelea kuhamasisha amani na utulivu.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Mahusiano ya Dini toka Kanisa la KKKT Songea, Grace Msuya amesema bila amani na upendo Tanzania haitakuwepo hivyo amesisitiza viongozi wa dini na waandishi wa habari kuwa chachu ya kuhubiri amani na utulivu wakati wote.

“Tukifanya kosa kwenye uchaguzi,tujue  tayari tumekosa amani,tusali na tumuombe Mungu atuchagulie viongozi ambao wanastahili ili  kuendeleza Tanzania’’,alisisitiza Msuya.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Oktoba 21,2020

                               

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.