Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Ruvuma limeendelea na kampeni yake ya matumizi salama ya nishati ya umeme, likiwaangazia wananchi wa mitaa ya Chandarua na Mitendewawa katika kata ya Mshangano, Manispaa ya Songea Mjini.
Diwani wa kata ya Mshangano, Samweli Mbano, ameishukuru TANESCO kwa jitihada zake za kuhakikisha wananchi wa mitaa hiyo wanapata huduma ya umeme, huku akifafanua kuwa jumla ya transfoma mbili zimefungwa ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora na endelevu kwa wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza kuhusu usalama na utunzaji wa miundombinu ya umeme, Afisa Habari na Uhusiano wa TANESCO mkoani Ruvuma, Allan Njiro, amekemea vikali vitendo vya wizi wa nyaya za umeme vinavyofanywa na baadhi ya watu, akisisitiza kuwa vitendo hivyo vinahatarisha maisha ya wananchi na kuvuruga huduma za umeme.
Njiro pia amewataka wazazi kuwa makini kwa kuhakikisha watoto hawachezi karibu na maeneo yenye transfoma za umeme ili kuepusha ajali, huku akisisitiza tahadhari wakati wa kukata miti iliyo karibu na nyaya za umeme.
Wananchi wa mitaa hiyo wameeleza kufurahishwa na huduma ya umeme waliyoipokea, wakilishukuru shirika la TANESCO kwa kuzingatia mahitaji yao na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia upatikanaji wa nishati ya umeme katika maeneo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.