• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TANROADS kujenga barabara ya Likuyu-Mkenda kwa kiwango cha lami

Imewekwa kuanzia tarehe: October 4th, 2022

WANANCHI wa vijiji  vinavyopitiwa na Barabara ya Likuyufusi –Mkenda na nchi jirani ya Msumbuji kwa upande wa mkoa wa Ruvuma,wameiomba Serikali kuanza ujenzi wa barabara  hiyo kwa kiwango cha lami ili kutatua changamoto za usafiri wa abiria na mizigo hususani katika kipindi cha masika.

Wametoa  ombi hilo kwa nyakati tofauti  mbele ya waandishi wa Habari wa mkoa wa Ruvuma walioko kwenye ziara  ya kutembelea miradi  ya barabara inayotarajia  kutekelezwa na inayotekelezwa na Serikali  ya awamu ya sita kupitia wakala wa barabara Tanzania(TANROADS) katika mkoa wa Ruvuma.

Shaban Kilomoni mkazi wa kijiji cha Nakawale wilayani Songea alisema,katika  wilaya hiyo kuna fursa nyingi ikiwamo makaa ya mawe,hata hivyo  bado hayajaanza kuchimbwa wala kunufaisha serikali kutokana na tatizo  kubwa la miundombinu ya barabara.

Alisema licha ya rasilimali nyingi zinazopatikana wilayani humo,wawekezaji na wafanyabiashara wameshindwa kufika kutokana na ubovu wa barabara hiyo,jambo linalochelewa  sana maendeleo yao.

“kukosekana kwa barabara ya lami ni chanzo cha kusua sua kwa maendeleo  kwenye maeneo yetu,hali hii imechangia sana hata usafiri  kwenda Songea mjini huwa ngumu siyo wakati wa masika tu bali hata  muda wa kiangazi, na madereva wanatumia nafasi hiyo kupandisha  nauli kutoka Sh.3000 hadi 7000”alisema.

Kandedus Mbawala dereva wa basi linalofanya safari zake kati ya Songea mjini na Mkenda darajani alieleza kuwa,wakati wa masika wanalazimika kutumia kati ya masaa 3 hadi 4 kufika Songea mjini  na kama ingejengwa kwa lami muda huo ungepungua hadi  saa 1.

Alisema kuwa,iwapo Serikali itajenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami  basi itaharakisha kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja,wilaya,mkoa na nchi kwa ujumla.

Hata hivyo, ameipongeza TANROADS kujenga barabara hiyo kwa  changarawe,hali iliyo rahisisha huduma ya usafiri na usafirishaji  kuendelea japo kwa shida wakati huu ambao serikali iko kwenye maandalizi ya kujenga kwa  kiwango cha lami.

Mrakibu wa Uhamiaji wa kituo cha Mkenda  Upendo Kikudo,alisema, watumishi wa serikali ni sehemu ya waathirika wakubwa  wa ubovu wa barabara hiyo kwani  wanapohitaji kwenda makao makuu ya wilaya na mkoa kikazi, wanalazimika kutumia muda mrefu na hivyo kuathiri shughuli za kuwahudumia wananchi.

Aidha,ameishukuru Serikali kwa kuonyesha nia ya kutaka kujenga barabara hiyo ambayo ni muhimu kwa uchumi wa nchi yetu na  nchi jirani ya Msumbiji.

Kwa mujibu wa Kikudo,barabara hiyo ni muhimu  na kama itajengwa kwa lami itatumika kikamilifu  kusafirisha bidhaa kutoka Bandari ya Mtwara kwenda nchi jirani ya Msumbuji kwa kutumia kituo cha  forodha cha Mkenda.

Alisema, kwa sasa wafanyabiashara wengi wa Msumbiji wanalazimika kutumia bandari ya Dar es slaam na  hatimaye kupita mpaka wa Tunduma mkoani Songwe unaounganisha Zambia na Tanzania,badala ya Bandari ya Mtwara na mpaka wa Mkenda na kwenda moja kwa moja nchini Msumbuji,hivyo kuwaongezea gharama kubwa.

Aliongeza kuwa, serikali itakapojenga barabara ya lami kutoka Likuyufusi hadi Mkenda km 124,kuna uwezekano mkubwa hata wa kujengwa  kituo  cha pamoja (One Stop Border Post)ambacho kitawezesha taasisi zote za serikali kuwa sehemu moja na kuwasiliana kwa haraka.

Kofi Binasi  raia wa Msumbuji,ameziomba Serikali za nchi hizo  kuunganisha nguvu na kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami ili kuharakisha uchumi na maendeleo ya watu wa nchi hizo.

Kwa upande wake Meneja wa wakala wa Barabara

Tanzania(TANROADS)mkoa wa Ruvuma Mhandisi Ephatar Mlavi alisema,Serikali iko mbioni kuanza ujenzi wa barabara  hiyo kwa kiwango cha lami na hadi sasa kazi iliyofanyika  ni upembuzi yakinifu.

Mlavi alisema kuwa,kwa sasa wako katika hatua za manunuzi kabla ya kumpata mkandarasi ambaye atajenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami na kumaliza kabisa changamoto ya usafiri  na kufungua uchumi wa mkoa wa Ruvuma.

Alisema Serikali kwa kutambua umuhimu wa eneo hilo kiuchumi, katika awamu ya kwanza itaanza  kujenga km 60 za kutoka Likuyufusi hadi Muhukuru na baadaye itaendelea kujenga km 64 hadi Daraja la Mkenda linalounganisha nchi ya Tanzania na Msumbiji.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.