• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TANZANIA na Ujerumani zakubaliana kurejeshwa mabaki ya Watanzania waliopoteza maisha wakati wa Ukoloni

Imewekwa kuanzia tarehe: October 31st, 2023

SERIKALI za nchi za Tanzania na Ujeruman zimesema zitafanya mazungumzo yatakayowezesha mabaki ya miili ya watanzania walipoteza maisha wakati wa ukoloni yaliyopo nchini Ujerumani yanarejeshwa nchini.

Kwa muda mrefu mabaki ya miili hiyo ya Watanzania imehifadhiwa katika makumbusho mbalimbali nchini Ujerumani na sasa uamuzi wa kuyarejesha umefikia hatua nzuri na hatimaye mabaki hayo yarejeshwe na kukabidhiwa kwa ndugu.

Ikumbukwe kwamba baadhi ya mabaki hayo ni ya miili ya machifu na viongozi waliokuwa vinara katika vita vya Tanganyika dhidi ya Ujerumani (Maji Maji).

Akizungumza leo Oktoba 31, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema katika mazungumzo yao wamezungumza masuala mbalimbali likiwemo kurejeshwa kwa mabaki hayo.

"Nakushukuru Rais Frank - Walter Steinmeier kwa kukubali mualiko wangu wa kuja kufanya ziara nchini, huu ni uthibitisho wa uhusiano mzuri kwa miaka miaka 60 baina ya nchi hizi.

"Katika mazungumzo yetu tumejadili masuala mbalimbali lakini tumezungumzia kuhusu mabaki ya wapendwa wetu walioko Ujerumani , tunaendelea kuzungumza ili mabaki ya miili ya wapendwa wetu irejee nyumbani Tanzania.

Wakati anazungumzia mabaki hayo , Rais Dk.Samia amesema anajua kuna familia ambazo zinasubiri mabaki ya miili ya ndugu zao ambayo yapo kwenye makumbusho za Ujerumani, lakini sasa wanakwenda kuyazungumza ili yaweze kurudishwa Tanzania.

Akielezea zaidi kuhusu mazungumzo kati yake na Rais Steinmeier, Rais Samia amesema wamezungumza kuhusu kuendelea kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili sambamba na kushirikiana katika nyanja mbalimbali kama elimu, afya, uhifadhi , kilimo, sekta ya ubunifu na maeneo mengine ambayo wamekuwa wakishirikiana.

Aidha Rais Samia ameishukuru nchi ya Ujeruman kwa misaada mbalimbali waliyoitoa na wanayoendelea kuitoa kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali akitolea mfano kuwa katika eneo la Bima ya Afya kwa Wote nchi hiyo iliahidi kusaidia lakini wanaendelea na ujenzi wa hospitali kubwa Dodoma.

"Ujeruman wamekuwa wakitusaidia katika maeneo mbalimbali, mbali ya ujenzi wa hospitali pale Dodoma lakini Ujeruman wametusaidia kujenga Hospitali Lugalo.Pia wamekuwa wakitusaidia katika uhifadhi katika hifadhi ya Serengeti na Selous.

Kwa upande wake Rais wa Ujeruman Steinmeier amemshukuru Rais Dk.Samia kwa kumualika kufanya ziara nchini huku akielezea namna ambavyo wamekuwa na mazungumzo mazuri yanayolenga kuimarisha uhusiano na kushirikiana katika sekta mbalimbali.

Kuhusu mabaki ya miili ya watanzania yaliyoko nchini Ujeruman amesema hilo ni jambo ambalo linazungumzika na watafikia pazuri huku katika hilo litaambatana na kupeleka Ujerumani taarifa za hali za wahanga wa vita vya majimaji ambao natarajia kukutana nao kesho.

" Nitakwenda kukutana na wahanga wa vita , nitawasikiliza na yale ambayo watanieleza nitakwenda nayo Ujeruman ili kufikisha ujumbe wao, "amesema huku akieleza ni vema pia nchi hizo kutosahau historia ya mambo yaliyopita na kubwa zaidi kudumisha uhusiano

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.