• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TARURA Songea inavyojivunia miaka miwili ya Rais Samia madarakani

Imewekwa kuanzia tarehe: March 20th, 2023

WAKALA wa Barabara za vijijini na mijini TARURA wilaya ya Songea,katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita imepokea jumla ya shilingi bilioni 19,190,960,200.2 kwa ajili ya kujenga,kukarabati na kufanya matengenezo ya miundombinu ya barabara.

Meneja wa TARURA wilaya ya Songea Mhandisi Bakari John alisema, kati ya fedha hizo shilingi bilioni 10,437,504,253.41 sawa na asilimia 254 zimetolewa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na shilingi bilioni 8,753,455,946.79 sawa na asilimia 196 ni za mwaka wa fedha 2022/2023.

Bakari alisema,ongezeko la fedha hizo ni kutoka serikali kuu kutokana na tozo ya shilingi 100 kwa kila lita moja ya mafuta(dizeli na petrol),fedha za mfuko wa  barabara na mfuko wa jimbo.

Amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili ya uongozi wake na kumshukuru kwa kuweza kuongeza fedha kwenye bajeti ya Tarura wilaya ya Songea kwa asilimia 196 kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Alisema,fedha hizo zimesaidia sana kuchochea shughuli za uchumi na kurahisisha usafiri na usafirishaji na kuongeza uboreshwaji wa mtandao wa barabara za vijijini na mijini hasa katika wilaya ya Songea.

Alisema,ongezeko  hilo la fedha imewezesha  hali ya barabara kuimarika na kuboreshwa kwa kiwango cha lami,changarawe,udongo,ujenzi wa vivuko na madaraja ili ziweze kupitika kipindi chote cha mwaka.

Kwa mujibu wa meneja huyo wa TARURA ni kwamba,kabla Rais Dkt Samia  Hassan kuingia madarakani bajeti ya Tarura wilaya ya Songea ilikuwa wastani wa shilingi bilioni 2,952,263,000.00 tu kwa mwaka.

Bakari alisema katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Dkt Samia,Tarura wilaya ya Songea imepata mafanikio  makubwa ikiwemo kuongezeka kwa barabara za lami kutoka kilomita 51.47 hadi kilomita 58.57.

Aidha alisema,barabara za changarawe zimeongezeka kutoka kilomita 345.70 hadi kilomita 457.17,barabara za udongo zimepungua kutoka kilomita 1,803.416 hadi kilomita 1,684.846 na idadi ya madaraja yaliyojengwa imeongezeka kutoka 125 hadi 150 na taa za barabarani kutoka 340 hadi 383.


Alisema,TARURA inaendelea kutekeleza miradi ya kimkakati kwa kufungua barabara ili kufika kusikofikika,kuboresha barabara zilizopo,kusaidia maeneo yote kufika  kwa wakati,kuunganisha huduma za usafiri wa barabara ndani ya wilaya,kupunguza gharama za uendeshaji wa vyombo vya moto,muda wa kusafiri na kufanikisha malengo  na maono ya wakala.

Moses Nyilenda mkazi wa Songea,ameipongeza serikai ya awamu ya sita kwa kuendelea kufanya maboresho makubwa ya miundombonu ya barabara za mitaa katika wilaya ya Songea na mkoa wa Ruvuma.

Alisema maboresho  hayo,yamesaidia barabara nyingi za mitaa katika manispaa ya Songea na maeneo ya vijijini kupitika kwa urahisi na kupanda thamani ya ardhi na amewaomba wananchi wenzake kutunza barabara hizo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na kurahisisha shughuli mablimbali za kiuchumi.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.