• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TFS Kusini yapanda miti milioni 4.3

Imewekwa kuanzia tarehe: May 23rd, 2022

ZAIDI ya miti milioni 4.3 imepandwa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS)kanda ya kusini kuanzia Mwezi Disemba hadi April 2022 huku miti takribani milioni 2 ikigawiwa kwa taasisi za Serikali ikiwamo shule za msingi,Sekondari na Wananchi.

Hayo yamesemwa jana na Kamanda wa TFS Kanda ya Kusini Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Uhifadhi wa misitu Manyise Mpokigwa,wakati akizungumzia kuhusu kampeni ya upandaji miti inayofanywa na TFS katika mikoa ya Kusini.


Mpokigwa alisema,kanda ya kusini yenye mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma ina mashamba ya miti ambako katika mkoa wa Ruvuma mashamba hayo ni Wino na Mpepo ambako wameotesha miti laini kwa ajili ya kupandwa katika mashamba yao na kugawa kwa taasisi za Serikali.

Alisema, TFS inasimamia aina mbili za misitu ambayo ni miti ya kupandwa na miti ya asili ambapo katika mkoa wa Ruvuma asilimia kubwa ya miti ni ya kupandwa ikilinganishwa na mikoa ya Lindi na Mtwara ambayo miti yake ni ya asili pamoja na miti michache ya kupandwa inayostahimili sana katika ukanda wa joto kama vile mitiki.

Alisema,katika bustani ya miti Ruangwa mkoani Lindi miti iliyozalishwa iligawiwa kwa Halmashauri zote zilizopo katika mkoa huo na wananchi na katika bustani ya Newala mkoani Mtwara miche iliyozalishwa kwa wingi ni ya matunda,miti ya vivuli,mitiki,mkongo na mpingo.

Alisema,TFS inapanda miti kwa malengo mbalimbali kama kurejesha uoto mahali ulipopotea,kubadili mitazamo ya watu kuhusu misitu na miti na wanahimiza jamii kupanda miti ili kupata mazao ya miti toka vyanzo vyao kwa ajili ya kupunguza kutegemea misitu ya asili.

Alisema,wana jukumu la kusimamia na kulinda rasilimali za misitu kwa ajili ya faida ya vizazi vya sasa na vinavyokuja,hivyo ni jukumu ya kila Mtanzania kupanda miti iwe ya mbao,matunda au kivuli kwani kufanya hivyo kutasaidia sana uwepo wa misitu ambayo faida zake ni nyingi.


Alisema,kuna sababu kwa Watanzania kuendelea kupanda miti katika maeneo mbalimbali ili kukabiliana na kasi ya uharibifu wa mazingira inayoendelea kufanywa na baadhi ya watu.

Alisema, katika msimu wa mwaka 2020/2021 jumla ya miche ya miti milioni 4 kati ya hiyo miche zaidi ya milioni 2 iligawiwa kwa wananchi na taasisi za Serikali na Dini kama mkakati wa TFS kupanda miti kibiashara.

Alisema, tathimini ya maendeleo ya miti iliyopandwa mwaka 2020/2021 iliyofanyika hivi karibuni imebaini kuwa, miti mingi iliyogawiwa na kuoteshwa na wadau mbalimbali imeota vizuri kwa asilimia 75 na michache imeshindwa kuota kutokana na hali ya hewa.

Alieleza kuwa,ile iliyopandwa kwenye taasisi kama shule ilishindwa kuendelea kutokana na janga la Covid-19 ambapo wahudumiaji ambao ni wanafunzi hawakuwepo shuleni hivyo kushindwa kuhudumiwa vizuri.


Alisema,katika kazi zao wanashirikiana kwa karibu na jamii na taasisi za Serikali ambapo mwaka 2021 TFS ilitoa zaidi ya mizinga 50 ya nyuki kwa wananchi katika Tarafa za Mchinga na Mtama.

Alisema, mizinga hiyo imetumika kama sehemu ya kuzuia wanyama waharibifu kama Tembo wanaovamia mashamba na kuharibu mazao na kuvuna asali kwa ajili ya kuwapatia wananchi kipato.

Alisema, katika wilaya ya Songea mkoa wa Ruvuma wamegawa mizinga ya nyuki 100 kwa vikundi vinne vinavyojihusisha na ufugaji nyuki katika maeneo mbalimbali.




Alisema, katika kusaidia maendeleo ya kijamii TFS kwa mwaka huu wa fedha hadi kufikia Mwezi Machi 2022, imetumia Sh.milioni 600 kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii na kutoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh.milioni 1.5.


Aidha alisema, TFS imetoa zaidi ya mbao 200 kwa taasisi za umma ikiwamo shule za msingi na sekondari na miche ya miti kwa ajili ya kurudisha uoto wa asili ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuzuia uharifu wa mazingira.


Kamishina Mpokigwa alisema,katika majukumu yao changamoto kubwa ni wananchi kuvamia misitu na kukata miti ovyo bila kufuata taratibu na sheria za nchi.


Mpokigwa alitaja changamoto nyingine ni uchomaji miti moto hasa nyakati za kiangazi kutokana na wananchi kufanya shughuli zao kama vile kuandaa mashamba, jambo linalo sababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na upotevu wa misitu ya asili.


Pia alisema,uvunaji haramu wa miti unaofanywa na wafanyabiashara wa mkaa wanaotumia baiskeli ambao wanatumia njia zisizo rasmi ni kati ya changamoto kubwa.

Kamanda Mpokigwa,ameziomba Serikali za vijiji na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kusaidiana katika kupambana na uvunaji haramu ya misitu.


“Wananchi wetu lazima wafahamu kwamba misitu ni rasilimali za nchi,hivyo zinapaswa kutumika kwa manufaa ya jamii nzima badala ya watu wachache”alisema Mpokigwa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.