Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Mkoa wa Ruvuma imegawa sukari kwa shule tano za Sekondari tano za Mkoa wa Ruvuma.
Sukari iliyogawiwa katika shule hiyo imekamatwa wakati ikiingizwa Nchini kwa magendo wilayani Nyasa kutoka Nchi jirani ya Malawi.
Akizungumza kwenye hafla ya ugawaji sukari hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Mbinga ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyasa MHE Aziza Mangosongo ameipongeza TRA kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili serikali ipate mapato halali.
Wakuu wa shule waliokabidhiwa Sukari ni kutoka sekondari za Mbamba bay, Kigonsera,Sekondari ya Wavulana Songea,sekondari ya Wasichana Songea,na sekondari ya Sekondari Tunduru . Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma Nicodemus Mwakilembe amesema wameamua kugawa katika shule tano za bweni ambapo kila shule imepata Mifuko 54 ya kilo 20.
Awali Akitoa Taarifa ya upatikanaji wa sukari hiyo ya magendo, Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma bw, Nicodemus Mwakilembe amesema Sukari hiyo ilikamatwa katika sehemu iliyohifadhiwa ili isafirishwe, sehemu mbalimbali hapa nchini na imeingizwa kwa magendo kutoka Nchi ya Malawi. Amefafanua kuwa, kwa kuwa sukari ilikuwa haina vibali sharia inawataka kutaifisha na kutumiwa sehemu mbalimbali kama vile shule na mara baada ya mapendekezo ya vikao halali wameamua kugawa katika shuleza 5 za bweni na Kila shule imepata Mifuko 54 ya kilo 20.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.