• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TUNDURU wanavyotumia michezo kuhamasisha sensa

Imewekwa kuanzia tarehe: August 19th, 2022

WAKAZI wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,wameshiriki katika Bonanza maalum la kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo na Watanzania  kujiandaa kushiriki kikamilifu zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika tarehe 23 mwezi huu nchini kote.

Bonanza hilo maarufu kwa jina la SAMIA SENSA BONANZA-TUNDURU limeshirikisha michezo mbalimbali ya matembezi ya  hiari umbali wa km 7,mpira wa miguu,bao,drafti,mpira wa wavu,kukimbiza kuku na rede  kwa wasichana ambapo washiriki wametoka kata zote 39  za wilaya ya Tunduru.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Bonanza hilo Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro,amewataka wananchi kujiandaa kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa na makazi  ili kuiwezesha serikali kupanga maendeleo,kupunguza umaskini na kukuza uchumi wa nchi yetu.

“matokeo ya sensa ya mwaka huu itasaidia serikali kupata taarifa na takwimu sahihi za wananchi wake na kupanga mipango ya maendeleo hasa ikizingatiwa kuwa,  katika sensa ya mwaka 2012 wilaya yetu haikufanya vizuri kutokana na  baadhi ya wananchi kutoshiriki zoezi hilo muhimu”alisema.

Amewaomba Wananchi, kutoe ushirikiano kwa watu waliopewa kazi ya kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali ili  zoezi hilo liweze kufanikiwa kama ilivyopangwa na Serikali.

Mtatiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usalama amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali wilayani humo, kuendelea kutoa elimu ya umuhimu wa sensa kwa wananchi ili kuwaweka tayari kushiriki zoezi hili muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Amewashukuru wakazi wa Tunduru hasa vijana  na watu wengine waliofika  kushuhudia Bonanza la Samia Sensa-Tunduru lililofanyika katika uwanja wa michezo wa CCM Tunduru mjini kuacha shughuli zao na kushiriki katika Bonanza hilo.

Kwa mujibu wa Mtatiro,Bonanza hilo ni mwanzo wa kuanza kwa Ligi ya Samia Sensa Bonanza-Tunduru  ambayo itafanyika kuanzia ngazi ya vijiji,kata,tarafa  na baadaye ngazi ya wilaya ambayo itatumika kwa kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi  pamoja na kuibua vipaji kwa vijana wa wilaya hiyo.Aidha katika Bonanza hilo, kulifanyika mechi ya hiari ya mpira wa miguu kati ya Timu  Ditram Nchimbi na Timu ya mwanamuziki wa kizazi kipya  Frank Ngumbuchi(FOBI) na Timu Ditram iliifunga Timu Fobi goli 1-0. goli lililofungwa na Ditram  Nchimbi dk 80.

Kwa upande wake Ditram Nchimbi,amewaomba Watanzania kujiandaa kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi na kuwataka wana michezo  na makundi mengine kuungana na Serikali  kuhamasisha wananchi kushiriki katika zoezi hilo.


Alisema,sensa ya watu na makazi ni muhimu sana kwani serikali ina lengo la kupata taarifa  sahihi za  idadi ya watu wake ili iweze kupanga mipango na kutoa hudumu za kijamii.

Naye Nahodha wa Timu ya Fobi  Frank Ngumbuchi(Fobi)alisema ataendelea kuiunga mkono serikali katika kufanikisha utekelezaji wa zoezi la sensa  na kuwaomba wakazi wa Tunduru na mkoa wa Ruvuma kuhakikisha kila mmoja anahesabiwa ili  serikali iweze kupata takwimu sahihi  na za uhakika wakati wa kupanga mipango ya maendeleo.
MWISHO.



 



 







Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.