• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TUNDURU yakusanya mapato kwa asilimia 106,yapata hati safi,RC Ibuge apongeza

Imewekwa kuanzia tarehe: June 23rd, 2022

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,ameipongeza Halmashsuri ya wilaya ya Tunduru, kwa kusimamia vizuri mapato na matumizi ya fedha za Serikali na kuiwezesha kupata hati safi katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Brigedia Jenereli Ibuge,ametoa pongezi hizo jana  wakati akizungumza na Madiwani  na watumishi wa Halmashauri hiyo katika kikao maalum cha Baraza  la madiwani cha kujadili taarifa za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali  kilicho fanyika kwenye ukumbi wa Klasta ya Walimu mjini Tunduru.

Alisema,Halmashauri ya Tunduru  imefanikiwa kukusanya jumla ya Sh.bilioni3,263,703,145 sawa na asilimia 106 kati ya lengo la kukusanya Sh.bilioni 3,076,638,496 kwa mwaka fedha 2020/2021.
Rc Ibuge alisema kuwa, mafanikio hayo yametokana na watumishi na madiwani kujisahihisha kwa makosa yaliyofanyika mwaka wa fedha 2020/2021 ambapo  Halmashauri hiyo ilipata hati yenye mashaka hali iliyotia doa kwenye rekodi zao za kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo.

Ibuge,amewaomba Madiwani na watendaji wa ngazi mbalimbali wa Halmashauri  hiyo, kuongeza bidii zaidi katika utendaji wao wa kila siku kwa lengo la kuhakikisha kuwa,hati safi zinaendelea kupatikana kwa kaguzi zijazo.
Amewapongeza madiwani na wadau wengine, kwa kuweza kuchangia kwa asilimia 100 mfuko wa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu  ambapo jumla ya Sh.milioni 409,946,884 zimetolewa.
Mkuu wa mkoa alisema, kati ya fedha hizo Sh.163,978,738  zimekwenda kwa vikundi 54 vya wanawake,Sh.163,978,738 kwa vikundi 53 vya vijana na Sh.81,989,369 zimetolewa kwa vikundi 34 kwa watu wenye ulemavu.


Alisema utelekezaji huo umeendana na maelekezo ya serikali ya awamu wa sita inayo sisitiza uwezeshaji wa jamii yote  ikiwamo makundi hayo maalumu ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

Aidha alisema,licha ya kupata hati safi lakini mwenendo wa ushughulikiaji wa Hoja,Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pamoja  na maagizo ya LAAC  katika Halmashauri hiyo unaridhisha kwa kiwango kikubwa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa ni kwamba, wakati wanajadili taarifa ya fedha ya mwaka 2019/ 2020 kulikuwa na hoja 26 ambazo zilikuwa bado hazijafanyiwa kazi pamoja na agizo 1 la LAAC.

Hata hivyo alisema,kati ya hoja hizo 26 za miaka ya nyuma hoja 23 zimehakikiwa na kufungwa,hoja zinazoendelea na utekelezaji ni 3 na agizo 1 la LAAC la miaka ya nyuma limetekelezwa na kufungwa.

Pia alisema, kwa upande wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2021 jumla ya hoja na mapendekezo Ishirini na nane aliyoyatoa CAG yamefanyiwa kazi kati ya hizo  kumi na saba yamefungwa baada ya uhakiki.

“huu ni mwenendo mzuri sana ,ninawapongeza kutokana na mnavyoshughulikia hoja na mapendekezo ya CAG katika Halmashauri yenu”alisema Ibuge.

Hata hivyo Balozi Ibuge, akatumia nafasi hiyo  kuwaagiza viongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanakamilisha utekelezaji wa majibu ya hoja  na mapendekezo 14, hoja 3 za miaka ya nyuma na 11 za mwaka wa fedha 2020/2022 kabla ya tarehe 30 Juni mwaka huu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro alisema,wamepokea viuatilifu vya zao la Korosho  kati ya hizo dawa za maji kwa asilimia 90 na upande wa dawa za Unga(Sulpher) wamepokea mifuko elfu 13,000 kati ya mifuko elfu 81 waliyopangiwa .

Akizungumzia hoja za mkaguzi mkuu na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali alisema kuwa, ana uhakika madiwani na wataalamu za Halmashauri hiyo watatekelezaji haraka kujibu hoja na mapendekezo yaliyobaki.

Awali  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Haillu  Mussa alisema, Madiwani kwa kushirikiana na wataalamu wa Halmashauri yake wamejipanga kujibu na kutekeleza maagizo na hoja zote  ili Halmashauri hiyo iendelee kupata hati safi mwaka hadi mwaka.
Mwisho.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.