UBORESHAJI wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Jimbo la Tunduru Kusini na Kaskazini linatarajiwa kuanza tarehe 28 Januari 2025 hadi 3 Februari 2025. Wananchi wote wanahimizwa kushiriki kikamilifu kwani kujiandikisha ni msingi wa uchaguzi bora.
Mafunzo ya kina kwa waandishi wasaidizi wa ngazi ya kata (ARO-Kata) yamekamilika kwa mafanikio makubwa. Mafunzo haya yamewalenga kuwajengea uwezo wa kutekeleza zoezi la uboreshaji wa daftari kwa ufanisi na kuzingatia viwango vya ubora.
Mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo hayo, Ndg. Chiza C. Marando, ametoa wito kwa watendaji kushirikiana kwa karibu ili kufanikisha zoezi hilo. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhari za ziada kwa kuwa jimbo hilo linapakana na nchi jirani, kuhakikisha kuwa waliojiandikisha ni raia halali wa Tanzania.
“Taratibu zote zilizowekwa na Tume zinapaswa kufuatwa, na vifaa vyote vya zoezi hili kutunzwa kwa makini,” alisema Ndg. Marando, akihimiza mshikamano miongoni mwa watendaji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.