• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UFUNGUZI rasmi maadhimisho ya siku ya UKIMWI Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: November 26th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahamed Abbas Ahamed, amesema kuwa Mkoa wa Ruvuma hali ya maambukizi imepungua kutoka asilimia 5.6 mwaka 2016/2017hadi kufikia asilimia 4.9  mwaka 2023 sawa na asilimia 0.7ya kiwango kilichopunguwa  ambapo halmashauri ya manispaa ya Songea inaongoza ikifuatiwa na halmashauri ya Tunduru.

Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo leo wakati akizindua Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani katika viwanja vya Michezo vya majimaji, ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Ruvuma katika Manispaa ya Songea mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philipo Mpango.

Kuhusu hali ya UKIMWI mkoani Ruvuma takwimu zinaeleza kuwa wanaoishi na maambukizi ya virus vya ukimwi (VVU) wapo 68,237 ambao wanaume ni 24,959 sawa na asilimia 37 ,Wanawake 43,000 sawa na asilimia 63 ,watoto chini ya umri wa miaka 15 wapo 2,382 sawa na asilimia 3.5 na watu wazima kuanzia umri wa miaka 15 wapo 65,855 sawa na asilimia 96.5.

" Ndugu viongozi pamoja na wananchi halmashauri zetu zinazoongoza ni maspaa ya Songea ikifuatiwa na Tunduru lakini vile vile na halmashauri ya Mbinga hivyo napenda kuchukuwa fursa hii kutoa wito kwa wananchi wote kuzingatia tiba na matunzo lakini vile vile kuendelea kutumia dawa za kufubaza kwani hiyo njia pekee ya kuendelea kupambana na matatizo haya" alisema Kanali Ahamed Abbas Ahamed.

Alisema kuwa siku hii  ya ufunguzi ni muhimu kwa kuelimisha umma kuhusu janga la UKIMWI, kuhamasisha kupunguza maambukizi mapya, na kuongeza juhudi za matibabu na huduma kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (VVU).

Katika uzinduzi huo, Kanali Ahamed alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa jamii, serikali, na wadau mbalimbali katika kupambana na ugonjwa huu. Hii ni sehemu ya jitihada za kitaifa kuendeleza elimu na ufahamu kuhusu UKIMWI, na kudumisha haki za watu wanaoishi na virusi hivyo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wizara ya Afya Dkt. Catherine Joachim Mkuu wa Program ameupongeza  uongozi wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na wananchi wake kwa kupiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi kwa ushamiri wa VVU umeshuka kutoka asilimia 5.6 mwaka 2016/17 mpaka asilimia 4.9 mwaka 2022 .

Alisema kuwa takwimu hizo zinaonesha Mkoa wa Ruvuma unaongoza katika upimaji wa VVU hata hivyo Mkoa umeendelea kufanya vizuri katika VVU vya 95/95/95 ambapo ushamiri wa utafiti wa mwaka 2023 tumeonesha asilimia 82 ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wanatambua hali zao za maambukizi na asilimia 97 ya walioambukizwa wanatumia dawa za kufubaza virusi vya ukimwi na asilimia 99 ya wanaotumia dawa za kufubaza tayari wameshafubaza virusi jambo ambalo linaoneaha Mkoa huo umepiga hatua kubwa sana ikili ganishwa na mwaka 2016/17.

" Japokuwa Mkoa upo nyuma ukilinganisha na wastani wa Kitaifa wa 95/95/95 ambapo 95 ya kwanza Kitaifa tupo asilimia 83, 95 ya pili tupo asilimia 98 na 95 ya Tau tupo asilimia 94" alisema Dkt. Catherine Joachm.

Alieleza zaidi kuwa kutokana na Mkoa wa Ruvuma umeendelea kukuwa kiuchumi kupitia shughuli za kilimo ,migodi ya makaa ya mawe na madini mengine, usafirishaji na uvuvi maendeleo hayo yamepeleta nakisi kubwa kwenye usawa unaopelekea baadhi ya makundi kuwa katika hatari zaidi ya maambukizi ya VVU.

Aidha alisema kuwa uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa Vijana wa kike kati ya miaka 15 na 24 wameendelea kuwa katika hatari hasa katika miji na vitongoji yanakopita maroli yakusafirisha makaa ya mawe kwenye machimbo madogo madogo na kwenye shughuli za uvuvi.

Naye Mwakilishi wa Baraza la watu wanaoishi na VVU na mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la NACOPHA Letisia Moris alisema kuwa hali ya unyanyapaa na ubaguzi wa VVU bado ni changamoto ndani ya Jamii hivyo uhathiri juhudi za kutokomeza Ukimwi wakati ni sawa kwa Kila Mmoja kuzingatia kauli mbinu ya mwaka huu inayoimiza juu ya mabadiliko ya tabia inayosema chagua njia sahihi ,tokomeza UKIMWI.

" Niwaombe viongozi wa dini, viongozi wa kimila na serikali kwa nafasi zao kuwa msatri wa mbele katika kukemea vitendo vya udhalilishaji ,unyanyapaa na ukatili kwa watu wanaoishi na VVU kwa kufanya hivi tutakuwa na Jamii iliyostaraabika na yenye uwelewa mkubwa wa namna ya kuheshimu haki za binadamu." Alisema Letisia

Hata hivyo ametia wito kwa wanaotunga Sera na mikakati ya kupambana na VVU kuzingatia vipaumbele vya Jamii hususani kwa Vijana katika utekwlezaji wa mipango ili kuharakisha upatikanaji wa matokeo chanya ifikapo mwaka 2030.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.