WAKULIMA wa zao la ufuta kutoka Halmashauri za Mbinga,Songea na Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wameuza kilo 352,774 za zao la ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani zilizowaingizia zaidi ya milioni 789.
Mnada huo umefanyika jana katika soko la kimataifa la nafaka lililopo OTC Lilambo Manispaa ya Songea ambapo Kampuni sita zilijitokeza kununua zao na kampuni ya Agro Processing ilishinda na kununua zao hilo kwa bei ya shilingi 2237 kwa kilo.
Akizungumza kabla ya ufunguzi wa mnada huo Mwenyekiti wa Kamati ya Mapato wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Martin Mtani amewashauri Wakulima wa zao la ufuta kukusanya na kuuza ufuta kwenye vyama vyao vya misingi (AMCOS).
Mtani amewashauri wakulima wapeleke ufuta na soya kwenye vyama vyo vya msingi ili yakauzwe kwa mfumo wa stakabadhi gharani, ambao unafaida kwa mkulima badala ya kuuza lejaleja.
“Hadi sasa tumefanikiwa kukamata magari manne ya mizigo yaliyobeba kilo 700 ambayo yalikiuka utaratibu wa kukwepa kulipa ushuru wa Halmashauri’’,alisisitiza Mtani.
Mtani ametoa onyo kali kwa wasafirishaji wa mazao ya mfumo wa stakabadhi ghalani kuacha kukwepa kulipa ushuru wa Halmashauri kwa kuwa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini ya shilingi laki mbili hadi million moja.
Katika msimu wa kilimo 2019/2020 Serikali haijatoa bei elekezi ya ununuzi na uuzaji wa mazao ya stakabadhi ghalani jambo ambalo ni faida kwa mkulima kwa sababu inawapunguzia tozo ya shilingi 133 ambayo imebebwa na mnunuzi na wao kubakiwa na tozo ya shilingi 171 ambayo ni gharama ya usafiri na vifungashio.
Imeandikwa na Jakline Clavery
Kaimu Afisa Habari Halmashauri ya Songea
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.