MKOA wa Ruvuma umefanikiwa kutoa wachezaji wawili waliochaguliwa kujiunga na timu ya Taifa ya wanafunzi ya Afrika Mashariki.
Hayo amesema Afisa Michezo Mkoa wa Ruvuma Antony Luoga kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na timu ya Taifa ni Longinus Mapunda kutoka Wilaya ya Songea na William Ngindo kutoka Wilaya ya Nyasa.
Luoga amesema kwa upande wa michezo ya UMITASHUMTA wamechaguliwa wanafunzi wawili kucheza timu ya Taifa akiwemo Fadhili Abdallah pamoja na Abdallah Mohamed wote wametoka Wilaya ya Tunduru.
Amesema Mkoa kwa michezo ya Shule ya Msingi na Sekondari mwaka 2021 Mkoa umeshiriki katika Mashindano yaliyofanyika Mkoa wa Mtwara ,Ruvuma haikufanya vizuri timu zilitolewa katika robo fainali.
“Mkoa wetu haukufanya vizuri timu zilitolewa hatua ya robo fainali na hivyo kushindwa kupata ushindi katika UMITASHUMTA”.
Hata hivyo amesema mashindano ya CHIMIWI mashindano hayo yanahusisha watumishi wa Serikali wa Wizara na Idara Serikali mwaka 2021 Mkoa wa Ruvuma ulipata ushindi wa kwanza katika mchezo wa bao.
Luoga ameelezea mashindano ya SAMIA Taifa Cup hujumuisha wananchi kwa ujumla yakiwa na lengo la kuibua vipaji ambavyo vitatumika katika Timu za Taifa na vilabu mbalimabli vinavyoshiriki ligi za Kitaifa.
“Katika mashindano hayo Mkoa wa Ruvuma umekuwa washindi wa Tatu katika mpira wa Miguu Kitaifa”.
Amesema Vijana wawili wa Sanaa ya Muziki wa kizazi kipya wamepata ufadhili wa masomo katika chuo cha sanaa Bagamoyo kwa muda wa mwaka mmoja na wanamichezo sita wamechaguliwa katika timu ya Taifa na vilabu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 14,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.