• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UTALII wa utamaduni unavyochangia kukuza utalii wilayani Nyasa

Imewekwa kuanzia tarehe: August 20th, 2024

Utalii wa utamaduni ni eneo lingine ambalo linachangia sana kukuza utalii wa mahali popote,Watu walioishi miaka mingi iliyopita Wilaya ya Nyasa walicheza ngoma mbalimbali zikiwa na lengo la kuburudisha, kuelimisha, kukosoa au kuwapongeza watu mbalimbali waliofanya mambo mazuri kwa jamii.

Mbunge wa Jimbo la Nyasa na Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya anataja moja ya ngoma hizo ni  Mganda,ngoma hii ilichezwa na wanaume na ngoma ya Kioda ambayo walicheza akina mama.Ngoma nyingine kama vile Lindeku, Mhambo, Lingoga na Chomanga walicheza mchanganyiko wanaume na wanawake.

Anasema katika utamaduni jamii za Nyasa zilialikwa kucheza ngoma za jadi nchi jirani za Msumbiji na Malawi, jambo ambalo hadi sasa bado linadumishwa la watanzania kualikwa kucheza ngoma Msumbiji au wa Msumbiji kualikwa Tanzania hasa vijiji vya mpakani kama vile Chiwindi.

Vyakula ni sehemu kubwa ya utalii,vyakula vya asili kwa wakazi wa Nyasa vimegawanyika katika makundi yafuatayo; chakula kikuu  ni ugali wa muhogo, mahindi, ulezi, mtama na ngano, vitoweo vimegawanyika katika makundi manne yafuatayo ambavyo ni samaki wakubwa na wadogo Pamoja na na dagaa.

Kundi la pili ni  mboga za majani ikiwemo mlenda, kisamvu, mchicha asili (libonongo), kundi jingine ni wadudu kumbikumbi, likungu, chenene (makururu), viyenje,mbambwa (majimoto) na  manganiwa.

Wilaya ya Nyasa pia ina pori ya akiba la wanyamapori la Liparamba ambalo lina wanyama wengi wakiwemo tembo, simba, chui, nyati, ngolombwe, parahala, tandala wakubwa, pundamilia, nyani manjano, pongo, Ngiri, pofu, kuro, fisi, nguruwepori na ndege jamii mbalimbali zaidi ya aina 80 ambao ni kivutio kizuri kwa watalii.

Wanyamapori hao wa Liparamba katika majira fulani ya mwaka wanatabia ya kuhama kwenda nchi jirani ya Msumbiji na baadaye hurudi tena kwenye pori la Liparamba kwa kuwa eneo hilo ni ushoroba wa wanyamapori.

Liparamba pia ni pori lenye maporomoko ya maji ya mto Ruvuma ambao umepita humo na unapokea maji kutoka mito miwili ya Lunyele na Lumeme ni kivutio kikubwa cha utalii na uwekezaji katika sekta.

Wilaya ya Nyasa ili iendelee kuwa kitovu cha utalii mkoani Ruvuma,uongozi unaendelea kulinda maeneo ya kihistoria na kiutamaduni kwa kushirikisha wananchi.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.