WAZIRI wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amefurahishwa na uwekezaji mkubwa katika shamba kahawa uliofanywa na Kampuni ya AVIV TANZANIA LTD katika kijiji cha Lipokela Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Kampuni hiyo inalima na kuchakata kahawa kwa mwaka tani zaidi ya 2000 katika shamba la kahawa lenye ukubwa wa hekta zaidi ya 1000.
Kahawa inayochakatwa na Kampuni hiyo inauzwa katika nchi mbalimbali zikiwemo Marekani.Saudi Arabia.India Japan,Jordan na Afrika ya Kusini.
Kampuni ya AVIV pia imetoa ajira za kudumu na za muda kwa wananchi wanaozunguka shamba hilo na wengine kutoka ndani ya Mkoa wa Ruvuma
Waziri wa Mipango na Uwekezaji alikuwa mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili Wilayani Songea .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.