• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

VIFO vya mama na watoto vyapungua Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: August 30th, 2023

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amezindua Mpango wa Usafirishaji wa Dharura kwa akinamama wajawazito,waliojifungua na Watoto wachanga (m-mama).

Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya hospitali ya Rufaa ya Mkoa  mjini Songea,Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankhoo,amesema mfumo huo utahakikisha vituo vya kutolea huduma za afya na wenye dharura wanapata usafiri wa dharura utakaopatikana wakati wote.

Amesema hadi sasa jumla ya madereva 140 kutoka katika Mkoa wa Ruvuma wametambuliwa, kuchaguliwa na kupata mafunzo maalum ya mfumo wa m-mama na kwamba wapo tayari kufanya kazi hiyo.

“Madereva hao watahusika kutoa huduma za usafiri wa dharura pale tu magari yetu ya kubeba wagonjwa yanapokosekana kwa sababu mbalimbali zinazoeleweka,muhimu ni kuhakikisha kila mama mwenye dharura anafikishwa  sehemu stahiki ili aweze kupata huduma bora kwa wakati’’,alisisitiza Mkuu wa Mkoa.

Kanali Thomas amesema mfumo huo ulizinduliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Aprili 6,2022 ambapo hadi sasa zaidi ya mikoa 19 nchini imekwishaanza kutekeleza mfumo wa m-mama ambapo Mkoa wa Ruvuma unaanza sasa kutekeleza mfumo huo ili kuboresha moja ya lengo kuu la Afya ya Huduma ya rufaa ya mama na mtoto.

Mkuu wa Mkoa amewaagiza wakurugenzi  kutekeleza mfumo huo katika Halmashauri zote,kuhakikisha kila mwaka bajeti ya usafiri wa dharura kwa wajawazito na Watoto wachanga inaingizwa katika mipango ya vituo vya kutolea huduma za afya na kufanya tathmini ya mahitaji ya vituo vyote vinavyotoa huduma za afya katika Mkoa.

Kwa upande wake Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Hilda Ndambalilo amesema Mkoa umepiga hatua katika kupunguza vifo vya akinamama vitokavyo na uzazi kutoka vifo 31 mwaka 2020 hadi kufikia  vifo 22 mwaka 2022.

Ndambalilo amesema vifo vya Watoto pia vimepungua kutoka vifo 326 mwaka 2020 hadi kufikia vifo 271 mwaka 2022 ambapo amesisitiza hatua mbalimbali kuendelea kuchukuliwa ili kupunguza idadi ya vifo vya mama na mtoto.

Amesema Mkoa umedhamiria kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha huduma bora zinapatikana ikiwa ni Pamoja na kuongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma za afya  za dharura za upasuaji kutoka vituo vya huduma 31 hivi sasa hadi kufikia vituo 35 ifikapo mwaka 2024.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Chihoma Mhako amesema Mkoa una magari 13 ya kubeba wagonjwa yanayofanya kazi ambayo yanatoa huduma za dharura kwa wagonjwa ambapo mahitaji ya Mkoa ni magari 38 hivyo Mkoa bado unakabiliwa na upungufu mkubwa  kwenye usafiri wa dharura.

Amesema kwa mwaka 2022 kulikuwa na jumla ya rufaa za dharura 1,306 za wajawazito zilizofanyika na kwamba zipo rufaa ambazo hazikupata mafanikio kutokana na kuchelewa kufika katika kituo cha huduma za dharura kwa wakati.

Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea Dr.Edson Fransis  amesema kuzinduliwa kwa mfumo wa m-mama,serikali imedhamiria kuokoa Maisha ya mama na mtoto na kwamba mradi utawezesha mama mjamzito,aliyejifungua na Watoto kupata huduma za haraka.

Amebainisha kuwa mgonjwa aanapobainika kuwa na tatizo atapiga simu ambayo itapokelewa na mtaalam katika hospitali ya Mkoa na kupata maelekezo ya kituo cha dharura cha Kwenda ili kupata huduma.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.