• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

VIJIJI vitatu Mbinga vinavyonufaika na maji ya RUWASA

Imewekwa kuanzia tarehe: December 6th, 2022

VIJIJI vitatu vya Amanimakoro,Mkeke na Paradiso katika Halmashauri ya Mbinga mkoani Ruvuma vimeanza kunufaika na miradi  miwili ya maji  inayosimamiwa na RUWASA iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 700.

Meneja RUWASA katika Wilaya ya Mbinga Mhandisi Mashaka Sinkala ameutaja mradi wa maji wa kwanza kuwa ni wa Amanimakro  unatekelezwa  na serikali kwa zaidi ya shilingi milioni 448.

Ameutaja mradi huo kuwa unahudumia vijiji vya  Amanimakoro,Mkeke na kitongoji cha Mkeso katika Kijiji cha Luhagara na kwamba vijiji vyote vina wakazi wapatao 5022 ambao wananufaika na mradi huo.

Hata hivyo amesema mradi huo wa maji ni miongoni mwa  skimu nne ambazo ni Amanimakoro, Lihale, Mkako na Kigonsera zinazosimamiwa na Jumuiya Jumuishi ya watumiaji maji ngazi ya jamii.

“Ili kuweza kukusanya maduhuri kwa ufanisi,Jumuiya inaendelea na uunganishaji wa maji kwa wateja majumbani sanjari na ufungaji wa dira za maji ambapo wateja 75 katika mradi huu tayari wameunganishiwa maji’’,alisema.

Amesema Jumuiya hiyo ni miongoni mwa Jumuiya tano katika Mkoa wa Ruvuma zinazofanya vizuri  katika  ukusanyaji maduhuri ambapo hadi sasa Jumuiya hiyo imeweza kukusanya zaidi ya shilingi milioni 10.

Ameutaja mradi mwingine wa maji kuwa ni unaotekelezwa katika Kijiji cha Paradiso chenye wakazi wapatao 1893 ambapo serikali kupitia RUWASA imetoa zaidi ya shilingi milioni 249 kutekeleza mradi huo ambao umeanza kutoa huduma za maji tangu Agosti 2021.

Mhandisi Sinkala ameutaja mradi huo kuwa ni miongoni mwa skimu za Jumuiya za Raunda, Kindimbajuu,Ntunduwalo,Paradiso na Ndongosi zinazosimamiwa na Jumuiya Jumuishi ya watumaji maji ngazi ya jamii katika kata za Raunda na Namswea.

Amesema Jumuiya hiyo inaendelea na uunganishaji wa maji kwa wateja na kwamba hadi sasa Jumuiya hiyo imeweza kukusanya maduhuri zaidi ya shilingi milioni 17 hadi kufikia Oktoba 2022.

Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegelo amewapongeza mameja wa RUWASA wilaya ya Mbinga na Mkoa wa Ruvuma kwa kusimamia vizuri miradi ya maji ambayo imeanza kuwahudumia wananchi.

Amesema RUWASA inaunga mkono kwa vitendo kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani na kwamba Rais amesema hataki kusikia ndani ya uongozi wake mama  anasafiri umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta maji.

“Kama kuna jambo ambalo Mheshimiwa Rais ataacha rekodi katika nchi hii ni katika eneo la maji ambayo yamekuwa kero kubwa hasa kwa mama na mtoto tangu nchi hii ipate uhuru’’,alisistiza Mhandisi Kivegelo.

Mbunge wa Jimbo la Mbinga vijijini Mheshimiwa Benaya Kapinga amempongeza Rais Samia kwa kutatua kero ya maji katika wilaya ya Mbinga hasa katika Kata za Amanimakoro na Kijiji cha Paradiso Kata ya Ruanda.

Ametoa rai kwa wananchi waliopokea miradi ya m aji kuendelea kuitunza miradi hiyo ili iwe endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Desemba 6,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.