Viongozi wa Majimaji AMCOS Waliojaribu Kumuhonga Mkuu wa Takukuru Tunduru wahukumiwa kulipa faini ya Milioni 1.5 na jela Miaka miwili
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya wa Tunduru mkoani Ruvuma imewahukumu viongozi wanne wa vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) kulipa faini ya shilingi milioni 1.5 na kifungo jela miaka miwili.
Viongozi waliohukumiwa ni Issa Rashid Makopi ambaye ni Mwenyekiti Majimaji AMCOS Tunduru, Mtuva Said Rashid ambaye ni Meneja Msaidizi Majimaji AMCOS,Mfaume Zuberi Mambo, Meneja Majimaji AMCOS na Halfa Said Chipangula Meneja Naluwale AMCOS.
Viongozi hao wamehukumiwa adhabu hiyo kutokana na kutoa hongo ya shilingi 800,000/= kwa Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Tunduru George Njogolo ili asiendelee na uchunguzi dhidi yao uliohusu ubadhilifu wa mbolea aina ya salfa inayotolewa bure na Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU LTD) kwa wakulima wa korosho waliopaswa kupewa na Viongozi hao kinyume na kifungu cha 15 (1) (b) na(2) vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [Sura ya 329 mapitio ya 2022.
Hukumu dhidi ya Viongozi hao ilitolewa Septemba 18,2024 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya Tunduru Bw. Shughuli J Mwampashe (SRM) akishirikiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw.Mwinyi Yahaya.
Washitakiwa wametiwa hatiani na Mahakama imewahukumu kulipa faini ya Shilingi Milioni 1.5 na kutumikia kifungo cha miaka miwili jela.Pia fedha kiasi cha shilingi 800,000/= kimetaifishwa na kuwa mali ya Serikali na kimewekwa katika akaunti ya Kamanda Uchunguzi Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.