Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Songea limewataka watendaji wa kata na Vijiji kuwajibika kusimamia miradi yote kikamilifu ambayo ipo katika maeneo yao
Agizo hilo nimetolewa na Baraza la Madiwani kwenye kikao cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha22/23 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Mkoani Ruvuma.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mhe, Menas Komba alisema wao kama baraza la madiwani hawapo tayari kuona Fedha za Serikali zikitumika vibaya kwa uzembe wa baadhi ya viongozi kutowajibika katika kusimamia miradi
Komba alisema niwajibu wa kila kiongozi wa kata katika Halmashauri hiyo kusimamia na kufuatilia matumizi sahihi ya fedha katika miradi yote inayojengwa kwenye maeneo yao kwani kama Halmashauri haipo tayari kupokea hati chafu kwasababu ya uzembe wa watendaji
“Lakini niwaombe waheshimiwa madiwani na viongozi wa kata mkasimamie majengo na mkayaelewe mamlaka yenu kama viongozi wa kata msikubali kuona miradi inayotekeleza na fedha za Serikali kupitia kodi za wananchi kujengwa chini ya kiwango” alisema komba.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Magembe amelihakikishia Baraza hilo la madiwani kuwa maagizo yote ya kikao hicho yatafanyiwa kazi kwa ufanisi mkubwa kwa kushirikiana na viongozi wa kata
“Ni kuhakikishie Mwenyekiti mbele ya baraza lako kuwa haya maagizo yote ni yakwetu tuingie kazini tukafanye kazi kwa maana hii inaonyesha wajibu wetu hatutekelezi vizuri hivyo niwasisitize watalamu turudi na majibu ya hiki tulichoelekezwa na baraza hili”alisema Magembe.
Maagizo hayo yamekatokana baada ya kusomwa kwa taarifa ya kamati ya fedha na mipango katika kikao cha baraza la madiwani ikionyesha baadhi ya miradi kutotekelezwa vizuri kwa kutosimamiwa ipasavyo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.